Pata taarifa kuu

Kashfa ya Phala Phala: Ramaphosa chini ya shinikizo, mkutano wa dharura wa ANC waitiswa

Mustakabali wa kisiasa wa rais wa Afrika Kusini haujafahamika. Mnamo mwezi Desemba, chama tawala kitateua wagombea wake kwa uchaguzi wa mwaka 2024.

Kwa miezi kadhaa, Bw Ramaphosa anakabiliwa na kesi ya wizi ya mwaka 2020 katika moja ya mali yake ya kifahari iitwayo Phala Phala (kaskazini mashariki), inayohusisha pesa za kushangaza zilizopatikana zimefichwa kwenye samani.
Kwa miezi kadhaa, Bw Ramaphosa anakabiliwa na kesi ya wizi ya mwaka 2020 katika moja ya mali yake ya kifahari iitwayo Phala Phala (kaskazini mashariki), inayohusisha pesa za kushangaza zilizopatikana zimefichwa kwenye samani. © AP/Nic Bothma
Matangazo ya kibiashara

Chama cha African National Congress (ANC) kimekutana kwa dharura siku ya Alhamisi nchini Afrika Kusini, siku moja baada ya kuwasilishwa kwa ripoti inayofungua njia ya utaratibu wa kufutwa kazi kwa mkuu wa nchi na rais wa chama tawala, Cyril Ramaphosa.

Kamati ya Utendaji ya Kitaifa yenye uwezo mkubwa katika uongozi wa chama "inakutana leo saa moja usiku", afisa mkuu wa ANC ameliambia shirika la habari laAFP, akiongeza kuwa majadiliano yatazingatia kashfa ya Phala.

Kwa miezi kadhaa, Bw Ramaphosa anakabiliwa na kesi ya wizi ya mwaka 2020 katika moja ya mali yake ya kifahari iitwayo Phala Phala (kaskazini mashariki), inayohusisha pesa za kushangaza zilizopatikana zimefichwa kwenye samani. Mkuu wa nchi anashutumiwa kwa kutoripoti tukio hilo kwa polisi au kwa mamlaka ya ushuru.

Siku ya Jumatano, tume huru iliyoteuliwa na Bunge ilitoa ripoti iliyohitimisha kwamba "rais anaweza kuwa amefanya" ukiukaji na makosa katika muktadha wa suala hili ambalo lilizuka kabla ya makataa muhimu ya uchaguzi kwa mustakabali wa kisiasa wa rais.

Siku moja kabla ya uchaguzi wa mchujo

Chama cha ANC inakutana kuanzia tarehe 16 hadi 20 Desemba ili kumteua kiongozi wake ajaye. Yeyote atakayeibuka mshindi atakuwa mkuu wa nchi mwishoni mwa uchaguzi mkuu wa 2024, ikiwa itashinda uchaguzi.

Cyril Ramaphosa, ambaye pia alighairi kipindi cha maswali na majibu kilichopangwa Bungeni wakati wa mchana, anakanusha mashtaka ya aina yoyote.

Bunge linakutana katika kikao kisicho cha kawaida siku ya Jumanne kuangazia mapendekezo ya ripoti hiyo ambayo haitakiwi kufuata lakini ambayo yanaweza kuliongoza kufungua mchakato wa kura ya kumshtaki mkuu wa nchi.

Jambo hilo linachafua taswira ya mkuu wa nchi, anayetarajiwa kuwa mstari wa mbele wa ufisadi ambao ameapa kuutokomeza.

Ofisi ya Rais ilitoa wito wa "kusoma kwa makini na kuzingatiwa ipasavyo" kwa ripoti ya tume "kwa maslahi ya utulivu wa serikali na nchi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.