Pata taarifa kuu

Mgomo wa kitaifa wa watumishi wa umma waitishwa Afrika Kusini

Vyama vya wafanyakazi wa umma nchini Afrika Kusini siku ya Alhamisi vimeitisha mgomo mkubwa nchini kote wiki ijayo kuhusu mishahara, mwezi mmoja kabla ya makataa muhimu ya mustakabali wa kisiasa wa Rais Cyril Ramaphosa.

Wanaharakati wa vyama vya wafanyakazi nchini Afrika Kusini waandamana mjini Pretoria dhidi ya mfumuko wa bei mjini Pretoria, Agosti 24, 2022.
Wanaharakati wa vyama vya wafanyakazi nchini Afrika Kusini waandamana mjini Pretoria dhidi ya mfumuko wa bei mjini Pretoria, Agosti 24, 2022. REUTERS - STAFF
Matangazo ya kibiashara

Chama tawala cha African National Congress (ANC) kinatazamiwa kukutana katikati ya mwezi wa Desemba ili kumchagua au la Ramaphosa kama mgombea kwa muhula wa pili katika uchaguzi wa rais wa 2024, kwa kumchagua tena kama kiongozi wa chama.

Vyama vya wafanyakazi vinavyowakilisha mamia kwa maelfu ya wafanyakazi wa sekta ya umma vimetangaza maandamano Jumanne ijayo mbele ya hospitali, bandarini na mbele ya majengo ya serikali.

Kutokana na kupanda kwa kasi kwa gharama ya maisha, serikali inataka watumishi wa umma kulipia ongezeko la chini ya mfumuko wa bei. Haiwezi kudumu," vyama vya wafanyakazi vimesema katika taarifa ya pamoja, wakitaka nyongeza ya 10%.

Mapema mwezi huu, Waziri wa Kazi Thulas Nxesi aliahidi 3%, kiwango ambacho kilichukuliwa kuwa "hakitoshi". Mfumuko wa bei nchini Afrika Kusini ulikuwa 7.5% mwezi Septemba, chini ikilinganishwa kilele cha 7.8% mwezi Julai.

Uchumi wa Afŕika Kusini hivi kaŕibuni ulikumbwa na matatizo makubwa kutokana na migomo ya wiki kadhaa katika huduma za reli na bandari, hali ambayo imeathiri mauzo ya nje ya madini na matunda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.