Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Watumishi wa umma wagoma wakidai mishahara

Maelfu ya watumishi wa umma wamefanya mgomo wa siku moja nchini Afrika Kusini siku ya Alhamisi kwa madai ya mishahara, kulingana na mashirika yaliungana na mgomo huo.

Uchumi wa Afrika Kusini tayari umeathirika pakubwa kutokana na migomo ya wiki kadhaa katika huduma za reli na bandari ambayo imeathiri mauzo ya nje ya madini na matunda.
Uchumi wa Afrika Kusini tayari umeathirika pakubwa kutokana na migomo ya wiki kadhaa katika huduma za reli na bandari ambayo imeathiri mauzo ya nje ya madini na matunda. Reuters
Matangazo ya kibiashara

 

Mgomo huo umeongozwa na moja ya vyama vikuu vya utumishi wa umma nchini Afrika Kusini, Public Servants Association (PSA), ambacho kina wanachama 235,000.

Mzozo kuhusu mishahara ya watumishi wa umma ulipamba moto baada ya Waziri wa Kazi, Thulas Nxesi kutangaza nyongeza ya 3% wiki jana, huku vyama vya wafanyakazi vikidai 6.5%. Wafanya kazi katika sekta za afya, huduma za uhamiaji na hata polisi wamejiunga a wenzao katika mgomo huo.

Kulingana na PSA, mgomo huo ulikuwa na "athari kubwa" kwa Wizara ya Mambo ya Ndani, uchukuzi na mamlaka ya forodha. Kulingana na muungano huo, "mtazamo wa waziri wa kutowajibika umeharibu mahusiano ya kijamii ambayo tayari ni magumu na kuzidisha ukosefu wa uaminifu" na washirika wa kijamii.

Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini Enoch Godongwana alisema alipotangaza bajeti ya mwezi Oktoba kwamba serikali inaweza kumudu tu nyongeza ya mishahara ya 3.3%, chini ya mfumuko wa bei ambao ulifikia 7.8%.

Uchumi wa Afrika Kusini tayari umeathirika pakubwa kutokana na migomo ya wiki kadhaa katika huduma za reli na bandari ambayo imeathiri mauzo ya nje ya madini na matunda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.