Pata taarifa kuu

Tabia nchi: Euro milioni 600 zatolewa kwa ajili ya mabadiliko Afrika Kusini

Ufaransa na Ujerumani zimetoa bahasha ya awali ya euro milioni 600 kwa ajili ya msaada wa mpito wa nishati nchini Afrika Kusini kama sehemu ya mpango wa uwekezaji ulioidhinishwa katika mkutano wa kilele wa COP 27 wa mabadiliko ya tabia nchi nchini Misri kwa jumla ya dola bilioni 98.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amerudia kukosoa nchi tajiri kwa kutoa misaada kwa nchi maskini zaidi hasa kwa njia ya mikopo ambayo inahatarisha kuongeza deni lao.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amerudia kukosoa nchi tajiri kwa kutoa misaada kwa nchi maskini zaidi hasa kwa njia ya mikopo ambayo inahatarisha kuongeza deni lao. © AP/Nic Bothma
Matangazo ya kibiashara

"Afrika Kusini, Ufaransa na Ujerumani zimesaini mikataba ya mkopo kwa mataifa hayo mawili ya Ulaya kwa kila moja kutoa euro milioni 300 katika ufadhili wa masharti nafuu kwa Afrika Kusini ili kuunga mkono juhudi za nchi hiyo kupunguza utegemezi wake wa makaa ya mawe," nchi hizo tatu zimetangaza katika taarifa yake ya pamoja. siku ya Jumatano.

Afrika Kusini inapata 80% ya umeme wake kutoka kwa makaa ya mawe, ambayo ni mhimili mkuu wa uchumi ambao unaajiri karibu watu 100,000. Mitambo kadhaa ya kuzalisha umeme itazimwa ifikapo mwisho wa mwaka 2030. Kampuni ya umma ya Eskom, ina madeni, haiwezi kuzalisha umeme wa kutosha pamoja na mitambo ya kuzeeka na inasababisha kukatika kwa umeme mara kwa mara.

Mpango wa uwekezaji wa dola bilioni 98 kwa ajili ya mpito wa nishati ya nguvu ya viwanda inayoongoza barani Afrika uliidhinishwa mapema wiki hii katika mkutano wa kilele wa COP 27 wa mabadiliko ya tabia nchi mjini Sharm el-Sheikh, uliofunguliwa Jumapili, baada ya makubaliano ya kimsingi yaliyofikiwa mwaka jana katika COP26 huko Glasgow.

Ufaransa, Ujerumani, Uingereza, Marekani na Umoja wa Ulaya ziliahidi kuunga mkono dola bilioni 8.5 kwa nia ya kuifanya Afrika Kusini kuwa mfano wa ushirikiano wa kuigwa katika vita dhidi ya hewa chafu katika nchi zinazoendelea.

Kitita kilichotolewa na Ufaransa na Ujerumani, katika mfumo wa mikopo kutoka kwa benki ya uwekezaji wa umma ya Ujerumani (KfW) na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), ni awamu ya kwanza ya msaada huu. Nchi hizo mbili zimeahidi kulipa euro bilioni moja kila moja kwa Afŕika Kusini, ambayo itahitaji angalau dola bilioni 500 kufikia hali ya kutoegemeza kaboni ifikapo mwaka 2050, kulingana na Benki ya Dunia.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amerudia kukosoa nchi tajiri kwa kutoa misaada kwa nchi maskini zaidi hasa kwa njia ya mikopo ambayo inahatarisha kuongeza deni lao.

Nchi za Kusini zitahitaji zaidi ya dola trilioni 2 kwa mwaka ifikapo 2030 kufadhili hatua zao za Tabia nchi, karibu nusu yao itatoka kwa wawekezaji wa nje, kulingana na ripoti iliyoagizwa na rais wa COP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.