Pata taarifa kuu
USALAMA-UGAIDI

Hatari ya shambulio: Pretoria yatupilia mbali onyo la Marekani

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa siku ya Alhamisi amesikitishwa na tahadhari juu ya hatari ya kutokea kwa shambulio mjini Johannesburg iliyotolewa siku moja kabla na Ubalozi wa Marekani nchini Afrika Kusini, ikitaja tahadhari hiyo kama ya "bahati mbaya".

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa.
Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa. Phill Magakoe / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Ni bahati mbaya kwamba Marekani inatoa onyo la aina hii bila kulijadili hata kidogo," amesema mkuu wa nchi wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Pretoria.

Ubalozi wa Marekani mjini Pretoria ulichapisha ilani kwenye tovuti yake Jumatano ikionya kwamba serikali yake "imepokea habari kwamba magaidi wanaweza kupanga kutekeleza shambulio linalolenga mikusanyiko mikubwa ya watu katika eneo la Sandton", kitongoji cha watu matajiri kaskazini mwa mki wa Johannesburg Jumamosi wiki hii.

"Aina yoyote ya onyo itatoka kwa serikali ya Afrika Kusini na ni bahati mbaya kwa serikali nyingine kutoa tishio kama hilo, ili kuzua hofu miongoni mwa raia wetu," Ramaphosa amewaambia waandishi wa habari.

Serikali "inafanya kazi usiku kucha ili kuthibitisha na kuangalia kwa karibu ujumbe huu ambao umetoka Marekani," ameongeza Rais Ramaphosa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.