Pata taarifa kuu

Ramaphosa anaongoza dhidi ya waziri wa zamani katika uchaguzi wa kiongozi wa ANC

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa yuko mbele sana, akikabiliana na mgombea mwingine pekee katika uchaguzi wa ndani wa kiongozi wa chama tawala cha ANC, waziri wake wa zamani wa afya Zweli Mkhize ambaye alitimuliwa kwa ufisadi.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anahitimisha kongamano la ANC Julai 31, 2022 huko Johannesburg.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anahitimisha kongamano la ANC Julai 31, 2022 huko Johannesburg. REUTERS - SIPHIWE SIBEKO
Matangazo ya kibiashara

Bw.Ramaphosa, 70, amepata sauti 2,037 katika matawi ya chama, jambo ambalo linamweka vyema mbele ya mpinzani wake, Zweli Mkhize, 66, ambaye amepata sauti 916, chama cha  ANC kimesema katika mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu yake huko Johannesburg.

"Haya ni majina mawili yanayopendekezwa kwa wadhifa wa kongozi wa chama," amesema Kgalema Motlanthe, rais wa zamani wa Afrika Kusini na mkuu wa kamati ya uchaguzi ya ANC.

Chama cha Nelson Mandela, madarakani tangu kuanzishwa kwa demokrasia nchini humo mwaka 1994, kilikutana katika mkutano wake kuanzia Desemba 16 hadi 20 kuwachagua viongozi wake.

Yule atakayeibuka mshindi atakuwa mkuu wa nchi baada ya uchaguzi mkuu wa 2024, ikiwa chama kitashinda kura. Katika chaguzi zilizopita za serikali ya mitaa, mwaka wa 2021, ANC ilishuka chini ya 50% kwa mara ya kwanza katika historia yake.

Uteuzi wa Bw. Ramaphosa, ambaye atawania muhula wa pili, unakuja wakati anakabiliwa na kesi mbaya ya wizi ambayo analaani kuwa ni ujanja wa kisiasa.

Anatuhumiwa kwa kuficha kiasi kikubwa cha pesa katika moja ya mali zake mnamo mwezi Februari 2020, na kuibua tuhuma za utakatishaji wa pesa na ufisadi, madai ambayo anakanusha.

Bunge litakutana Disemba 6 kuamua iwapo atalazimika kujibu tuhuma hizi.

Aliyekuwa Waziri wa Afya, Zweli Mkhize aliondoka serikalini mwaka 2021 kufuatia tuhuma za ubadhirifu katika muktadha wa mapambano dhidi ya UVIKO-19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.