Pata taarifa kuu
ETHIOPIA- USALAMA.

Asilimia 65 ya wapiganaji wa TPLF wameondoka kutoka mstari wa mbele wa mapigano

 Kamanda wa vikosi vya eneo la Tigray nchini Ethiopia, amesema karibu asilimia 65 ya wapiganaji wake wameondoka kutoka mstari wa mbele wa mapigano, mwezi mmoja tangu kutiwa saini kwa mkataba wa usitishaji mapigano.

Wapiganaji wa kundi la TPLF wakiwa katika eneo la  Amhara, Novemba ,9 ,2020
Wapiganaji wa kundi la TPLF wakiwa katika eneo la Amhara, Novemba ,9 ,2020 REUTERS/Tiksa Negeri//File Photo
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Jenerali Tadesse Worede, vikosi vyao vimeanza kuondoka katika maeneo waliyokuwa wanayakalia, ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji makubaliano ya mkataba wa amani.

Uongozi wa Tigray, kwa miezi kadhaa umekuwa ukikataa mwito wa Serikali kuu iliyowataka waondoke na kuacha kufanya mashambulio dhidi ya wanajeshi wa Serikali.

Kuondoka kwa wapiganani hawa kumekuja siku chache kupita baada ya mwezi uliopita pande zinazohasimiana kutiliana saini mkataba wa amani nchini Afrika Kusini.

Mapigano kati ya waasi wa Tigray na vikosi vya Serikali vinavyosaidiwa na wanajeshi wa Eritea, yamesababisha vifo ya mamia ya watu huku maelfu wakilazimika kuwa wakimbizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.