Pata taarifa kuu

Eritrea yajibu kufuatia maombi ya kuondoa jeshi lake kutoka Tigray

Takriban mwezi mmoja baada ya kutiwa saini kwa makubaliano ya amani ya Pretoria kati ya serikali ya Ethiopia na mamlaka ya jimbo la Tigray, ambayo yanatoa nafasi ya kuondolewa kwa "majeshi ya kigeni" kutoka jimbo hilo, jeshi la Eritrea bado lipo. Kulingana na vyanzo kadhaa, jeshi la Eritrea bado linajihusisha na dhulma dhidi ya raia. Kwa mara ya kwanza, Jumatatu, Novemba 28, serikali ya Eritrea ilijibu shinikizo la kimataifa lililotaka kuondoka kwa vikosi vyake nchini Ethiopia.

Rais wa Eritrea Issayas Afewerki, Septemba 14, 2019.
Rais wa Eritrea Issayas Afewerki, Septemba 14, 2019. AFP - EBRAHIM HAMID
Matangazo ya kibiashara

Kama kawaida, serikali ya Eritrea hadi wakati huo ilikuwa haijajibu hadharani kuhusu kutiwa saini kwa mikataba ya Pretoria na Nairobi, wala maombi ya kuondolewa kwa jeshi lake katika jimbo la Tigray. Lakini siku ya Jumatatu, waziri wa habari wa Eritrea hatimaye alivunja ukimya wa wiki tatu ili kutoa maoni yake kuhusu ujumbe wa Twitter kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani. Ujumbe huo unaribisha ukweli kwamba mpatanishi wa Umoja wa Afrika Olusegun Obasanjo, alimtembelea jimbo la Tigray siku ya Jumamosi, alibainisha "kwamba hakuna nchi ambayo inaweza kukubali kuwepo kwa nchi ya kigeni kwenye ardhi lake".

“Unafiki! ameshtumu mara moja Yemane Ghebremeskel, mshirika wa karibu wa mkuu wa nchi wa Eritrea Issayas Afewerki. "Miundo ya ulinzi kati ya mataifa huru ya Afrika haiko chini ya idhini ya awali au kura ya turufu na mataifa ya kigeni," alieleza. Kwa hiyo maana yake ni wazi: kuwepo au kutokuwepo kwa jeshi la Eritrea nchini Ethiopia kunategemea tu makubaliano kati ya Eritrea na Ethiopia, na hakuna kitu kingine chochote.

Visa vya uporaji na watu wengi kuzuiliwa

Hata hivyo, ni ukweli kwamba, hadi sasa, Ethiopia haijaomba hadharani kujitoa nchini Ethiopia. Na wakati huo huo, katika maeneo ambayo bado inashikilia, jeshi la Eritrea limeshutumiwa kwa mauaji mapya ya raia katika siku za hivi karibuni. Shirika la habari la Associated Press (AP), likinukuu mashahidi na wafanyakazi wa mashirika ya misaada, limesema wanamgambo wa Amhara na wanajeshi wa Eritrea wanaendelea "kupora mali" katika mji wa kati wa Shire na "kuwakamata watu kiholela" huko Alamata, kusini mwa jimbo la Tigray.

Televisheni ya Tigray, kwa upande wake, imeripoti mashambulizi ya mabomu kwenye mji wa Irob, kusini. Naye mjumbe wa mamlaka ya Tigray katika mazungumzo huko Pretoria, Getachew Reda, mshauri wa rais wa jimbo hilo, amedai kuwa Waeritrea waliwanyonga makumi ya raia huko May Abay wiki iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.