Pata taarifa kuu

Mtazamo wa kiuchumi wa IMF unaotiwa wasiwasi kwa Afrika

Katika dokezo lililochapishwa Ijumaa hii, Oktoba 14, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) lina mtazamo mbaya kwa Afrika. IMF inabaini kushuka kwa ukuaji kutoka 4.7% mwaka 2021 hadi 3.6% mwaka huu na viashiria vingine vilivyobainishwa na taasisi hiyo pia vinazingatiwa kuwa vya kutia wasiwasi.

Nembo ya Shirika la Fedha la Kimataifa.
Nembo ya Shirika la Fedha la Kimataifa. AP - Andrew Harnik
Matangazo ya kibiashara

Ukosefu wa usawa wa uchumi mkuu umejitokeza tena, inabainisha IMF katika maelezo yake ya Ijumaa hii, Oktoba 14. Madeni ya umma na mfumuko wa bei uko katika viwango ambavyo havijaonekana katika miongo kadhaa. Hali hiyo inasababihwa na, usumbufu wa hifadhi na vita nchini Ukraine.

Mfumuko wa bei wa tarakimu mbili

Kutokana na machafuko hayo, mfumuko wa bei duniani na uwezekano wa kudorora kwa uchumi wa China, zaidi ya theluthi moja ya nchi za Afrika zinakabiliwa na mfumuko wa bei wa tarakimu mbili na watu wanaona uwezo wao wa kununua unapotea. Muktadha wa kiuchumi unaofaa kwa mivutano ya kijamii, inaonya IMF ambayo inathibitisha kwamba tunaingia "kipindi kipya cha kukosekana kwa utulivu na hatari za kuzorota kwa uchumi".

Mazingira ya sasa ya kiuchumi ni mojawapo ya magumu zaidi tangu miaka kadhaa, pia inabainisha IMF, ambayo itawashawishi viongozi wengi kupata "usawa wa kutosha". Hivyo, ili kuyasaidia mataifa haya, IMF inabainisha vipaumbele vinne vinavyotakiwa kutekelezwa ili kukabiliana na hali ya hatari iliyopo.

Na hilo huanza na mapambano dhidi ya uhaba wa chakula. Huku watu milioni 123 wakiwa tayari hawana uhakika wa chakula, kupanda kwa bei ya chakula na nishati kunaweka maisha ya watu wengi katika hatari zaidi. Kwa hiyo IMF inatoa wito wa kugeukia njia mbadala zinazolengwa na kusambaza rasilimali chache zinazopatikana kwa walio hatarini zaidi.

Jambo la pili lililoangaziwa na taasisi ya kimataifa: ujumuishaji wa fedha za umma katika muktadha wa hali ngumu zaidi ya ufadhili. Kwa hiyo anashauri mataifa kuongeza mapato, kuweka vipaumbele vya matumizi na kusimamia madeni kwa makini. Hii itahusisha hasa urekebishaji wa deni la baadhi ya nchi na utekelezaji bora wa mfumo wa pamoja wa G20.

Miundombinu thabiti

Kuhusu udhibiti wa mfumuko wa bei, IMF inaonya: kuongeza viwango vya riba lazima kufanywe kwa busara na taratibu.

Hatimaye, ili kuunda mazingira ya ukuaji endelevu na wa kijani kibichi katika muktadha wa mabadiliko ya Tabia nchi, ambayo tayari yana athari kubwa kwa idadi kubwa ya nchi za bara la Afrika, IMF inapendekeza kwamba mataifa yawekeze katika miundombinu thabiti na kutumia rasilimali nyingi na nishati mbadala katika ukanda huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.