Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Kesi ya kiongozi wa zamani wa waasi wa Afrika ya Kati yaanza ICC

Mshtakiwa huyo, Mahamat Said, amekana mashtaka. Viongozi wengine wawili wanaoshukiwa kuwa wanamgambo hasimu pia wako chini ya ulinzi wa ICC.

Mahamat Said Abdel Kani wakati wa ufunguzi wa kusikilizwa kwa uthibitisho wa mashtaka kwenye makao makuu ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mjini Hague tarehe 12 Oktoba 2021.
Mahamat Said Abdel Kani wakati wa ufunguzi wa kusikilizwa kwa uthibitisho wa mashtaka kwenye makao makuu ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mjini Hague tarehe 12 Oktoba 2021. © ICC-CPI
Matangazo ya kibiashara

Mshukiwa mkuu wa kundi la waasi la Jamhuri ya Afrika ya Kati lenye Waislamu wengi zaidi waliomuondoa madarakani Rais Francois Bozize mwaka 2013, amekana mashtaka saba ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu Jumatatu hii Septemba 26, 2022.

Msemaji wa mahakama amesema kufunguliwa kwa kesi ya Mahamat Said, 52, kunaashiria mwisho wa kusubiri kwa muda mrefu haki kwa waathiriwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Baada ya ofisa wa mahakama kusoma mashtaka hayo, yakiwemo mateso, kifungo kisicho halali na mateso, Said ameliambia jopo la majaji watatu, "Nimesikiliza yote mnayonituhumu lakini nasema sina hatia."

Anashutumiwa kwa kusimamia kituo cha kizuizini katika mji mkuu wa Afrika ya Kati, Bangui, kiitwacho Ofisi Kuu ya Kukandamiza Ujambazi (OCRB), kuanzia mwezi wa Aprili hadi Agosti 2013, ambapo yeye na waasi kadhaa wa Seleka wanadaiwa kuwashikilia wafungwa wanaoonekana kuwa wafuasi wa rais wa zamani François Bozize katika mazingira yasiyo ya kibinadamu. Wanadaiwa kuwatesa na kuwahoji kikatili, ikiwa ni pamoja na kuwachapa viboko na kuwapiga kwa marungu na mitutu ya bunduki, kwa mujibu wa upande wa mashtaka.

Mwanasheria Mkuu wa ICC, raia wa Uingereza Karim Khan, amesema Mahamat Saïd "hakuwa mtazamaji tu" wa uhalifu uliotendewa waathiriwa, lakini mshiriki hai. "Alijua ni nini hasa alikuwa amepanga kwa ajili yao, ni madhila gani yaliyowangojea chini ya udhibiti wake na chini ya ulinzi," mwendesha mashtaka amesema.

Seleka dhidi ya anti-balaka

Mashtaka dhidi yake yalianza wakati wa mapigano yaliyotokea mjini Bangui mwaka 2013 kati ya waasi wa Seleka na wanamgambo wa Kikristo hasa wanaoitwa Anti-balaka. Mapigano haya yalisababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwakosesha makazi mamia ya maelfu ya raia.

Mahakama ya Hague pia iliwaweka kizuizini makamanda wawili wa Anti-balaka, Alfred Yekatom na Patrice-Edouard Ngaïssona, ambao walihukumiwa pamoja.

"Kwa miezi kumi ya kutisha, Seleka ilitawala Bangui," Khan amesema. "Kusema kwamba walitawala itakuwa ni kosa. Walitawala kwa mfumo wa kiimla, kwa kutia uoga raia, kwa ugaidi," ameongeza.

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka, mashahidi katika kesi hiyo ni pamoja na watu walionusurika na watu walioshuhudia mateso hayo, wakiwemo waliokuwa wasaidizi wa Mahamat Said.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.