Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Adhabu ya kifo yafutwa Equatorial Guinea

Equatorial Guinea imetangaza kufuta adhabu ya kifo, miaka minane baada ya adhabu ya mwisho kutekelezwa nchini humo. 

Jiji la Malabo, mji mkuu wa Equatorial Guinea.
Jiji la Malabo, mji mkuu wa Equatorial Guinea. STR / AFP
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa kusitisha adhabu hiyo  imetangazwa na rais Teodoro Obiang, baada ya kutia saini sheria mpya za kukabiliana na makosa ya jinai nchini humo. 

Hatua hii imepongezwa na wanaharakati wa haki za binadamu nchini humo, kufuatia nchi hiyo ya Afrika ya Kati, kuwa na rekodi mbaya ya haki za binadamu. 

Tangu mwaka 2019, rais Obiang mwenye umri wa miaka 80,  ambaye amekaa madarakani kwa miaka 43 sasa, aliahidi kuondoa adhabu hiyo, baada ya mtu wa mwisho kupewa adhabu hiyo mwaka 2014. 

Makamu wa rais Teodoro Nguema Obiang Mangue, mtoto wa rais huyo  amesema hatua iliyochukuliwa na baba yake ni ya kihistoria na sasa itaanza kutekelezwa baada ya siku 90. 

Equatorial Guinea, inaugana na mataifa mengine 20 ya Afrika ambao yameondoa adhabu hiyo, lakini mengine zaidi ya 30 bado yanaitekeleza. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.