Pata taarifa kuu

Watu tisa wakufa maji katika ajali ya meli kwenye Mto Madagascar

Takriban watu tisa wamefariki baada ya meli mbili kugongana  kwenye mto Loza, karibu na mji wa Antsohihy, kaskazini-magharibi mwa Madagascar, mamlaka ya bahari imesema.

Mwezi Desemba, muda mfupi kabla ya Krismasi, watu 88, wengi wao wakiwa wafanyakazi wa msimu ambao walikuwa wamemaliza kuvuna karafuu na walikuwa wakirejea nyumbani, walifariki baada ya meli ya mizigo waliokuwemo kuzama kaskazini mashariki mwa Madagascar.
Mwezi Desemba, muda mfupi kabla ya Krismasi, watu 88, wengi wao wakiwa wafanyakazi wa msimu ambao walikuwa wamemaliza kuvuna karafuu na walikuwa wakirejea nyumbani, walifariki baada ya meli ya mizigo waliokuwemo kuzama kaskazini mashariki mwa Madagascar. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Majira ya saa kumi na moja jioni siku ya Jumapili, meli ya mizigo iliigongana na boti iendayo kasi iliyokuwa na watu 35, wakiwemo watoto, ambayo ilizama mara moja. Watu tisa walifariki kulingana na mamlaka hiyo, huku baadhi ya abiria waliweza kurejea ufuoni, kwa mujibu wa mashahidi.

"Bado haijulikani ni nini kilitokea kwa abiria wengine," Jean-Edmond Randrianantenaina, mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bahari na Bandari (APMF), ameliambia shirika la habari la AFP. Operesheni za uokoaji zinaendelea.

Mwezi Desemba, muda mfupi kabla ya Krismasi, watu 88, wengi wao wakiwa wafanyakazi wa msimu ambao walikuwa wamemaliza kuvuna karafuu na walikuwa wakirejea nyumbani, walifariki baada ya meli ya mizigo waliokuwemo kuzama kaskazini mashariki mwa Madagascar.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.