Pata taarifa kuu

Madagascar: Kumi na tisa wauawa wakijaribu kuingia katika kambi ya jeshi

Wanajeshi wa Madagascar wamethibitisha Jumanne kwamba waliwaua watu 19 wakati walipofyatulia risasi kundi la watu wenye hasira waliojaribu kuingia katika kambi yao kusini mashariki mwa kisiwa hicho siku ya Jumatatu, kufuatia tuhuma za utekaji nyara wa mtoto albino.

Wanajeshi wa Madagascar walitangaza Jumatatu katika ripoti yao ya awali vifo vya watu 11.
Wanajeshi wa Madagascar walitangaza Jumatatu katika ripoti yao ya awali vifo vya watu 11. AFP - RIJASOLO
Matangazo ya kibiashara

"Watu 19 walipoteza maisha na majeruhi 21 wanaendelea kutibiwa" katika hospitali ya Ikongo, mji mdogo ambako makabiliano kati ya wandamanaji wenye hasira na wanajeshi, wanajeshi hao wamesema katika taarifa yao na kuongeza kuwa uchunguzi unaendelea.

Daktari mkuu wa hospitali ya eneo hilo, Dk Tango Oscar Toky, aliyewasiliana kwa simu na shirika la habari la AFP siku ya Jumanne, amesema watu 19 waliuawa kwa risasi.

Wanajeshi hao, ambao wanadai kuwa utulivu sasa umerejea, walitangaza Jumatatu katika ripoti yao ya awali vifo vya watu 11.

Washukiwa wanne wamekamatwa na kwa sasa wanazuiliwa na vikosi vya usalama .

Lakini wakazi wenye hasira wamedhamiria kujichukulia sheria mkononi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.