Pata taarifa kuu
madagascar

Idadi ya vifo nchini Madagascar yaongezeka hadi 85

Idadi ya vifo vilivyotokana na kuzama kwa boti ya mizigo inayojulikana kwa jina la Francia siku ya Jumatatu wiki hii imeongezeka hadi 85. Boti hiyo ilikuwa ikisafirisha bidhaa kaskazini-mashariki mwa Madagascar. Miili mingine imepatikana kulingana na mamlaka ya baharini na vikosi vya si vya usalama.

Ajali hiyo ilitokea kwenye pwani ya kaskazini-mashariki mwa Madagascar.
Ajali hiyo ilitokea kwenye pwani ya kaskazini-mashariki mwa Madagascar. AFP - ROBERTO SCHMIDT
Matangazo ya kibiashara

"Idadi ya waliofariki imeongezeka hadi 85, ikiwa ni pamoja na miili 21 iliyopatikana jana" (Jumatano), Mkuuu wa vikosi vya usalama Zafisambatra Ravoavy ameliambia shirika la habari la AFP.

Idadi ya abiria waliokuwemo ndani ya boti hii ya mbao yenye urefu wa mita kumi na mbili pia imeongezwa, hadi abiria 138, ambapo 50 pekee ndio wameokolewa, mamlaka ya baharini imesema.

Boti hiyo, ambayo haikuruhusiwa kupakia abiria, ilikuwa imeondoka katika mji mdogo wa Antseraka kuelekea Soanierana-Ivongo, karibu kilomita mia moja zaidi kusini mwa nchi. Ilizama karibu na eneo ambalo ilitarajiwa kuegesha.

Abiria wengi walikuwa wafanyakazi wa msimu, ambao walikuwa wametoka kuchuma karafuu na walikuwa wakielekea nyumbani kwa msimu wa likizo.

Serikali ya Madagascar imetangaza siku moja ya maombolezo ya kitaifa, na bendera zimepandishwa nusu mlingoti kote nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.