Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-UTALII

Madagascar yafungua tena mipaka yake kwa wasafiri kutoka Ulaya

Baada ya watalii kutoka Bahari ya Hindi wiki mbili zilizopita, Madagascar imefungua tena mipaka yake kwa wasafiri kutoka Ulaya, baada ya abiria 640 waliosafiri kwa ndege kutoka Paris kutua kwenye uwanja wa ndege wa Antananarivo.

Mtalii anatembea ufukweni kwenye kisiwa cha Nosy Be, Madagascar.
Mtalii anatembea ufukweni kwenye kisiwa cha Nosy Be, Madagascar. AFP - RIJASOLO
Matangazo ya kibiashara

Kwa karibu miezi 20, Madagascar ilikuwa imefungwa kwa wasafiri kutoka mataifambalimbali duniani, isipokuwa kwa raia wanaorejeshwa makwao. Hatu ya kufungua tena nchi hiyo kwa wageni iliombwa kwa miezi mingi na sekta ya utalii, moja ya sekta zilizoathiriwa zaidi na janga la Covid-19.

 

Hata hivyo Mamlaka nchini Madagascar imechukua hatua kadhaa kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona kama vile vipimo vya PCR kwa wasafri waonaoingia nchini na kuwekwa karantini kwa kipindi cha siku mbili katika hoteli mara tu wanaposhuka kwenye ndege.

"Zoezi hilo litafanyika hatua kwa hatua, lakini ni furaha kubwa kwetu" , amesema Jean-Théophile Randrianarijaona, mùkuu wa kitengo cha Utalii katika shirika la Airtours.

Katika kuzuia wimbi jipya la Covid-19 nchini, sekta ya Utalii pia imeomba wasafiri kupewa chanjo zaidi.

"Tunalazimika kukabiliana ili kuziba pengo, ambalo sasa linakadiriwa kufikia hadi dola milioni 900," amesema Jonah Ramampionona, kiongozi wa shirika la Airtours.

Ujio wa watalii ambao umechelewa kwa muda mrefu unasubiriwa huko Nosy Be, kisiwa kidogo kilicho kaskazini-magharibi mwa Madagascar. Wakazi wanaoishi huko hasa kutokana na utalii wanajutia kuendelea kufungwa kwa uwanja wao wa ndege kwa safari za ndege za kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.