Pata taarifa kuu
MADASCAR-CORONA-AFYA

Covid-19: Rais wa Madagascar Andry Rajoelina atangaza hatua mpya

Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina, ametangaza hatua mpya za kukabiliana na janga la Corona ambalo limesababisha vifo vya watu 148 nchini humo, baada ya vifo vipya 6 kuthibitishwa katika muda wa saa 24 zilizopita.

Rais wa Madagascar Andry Rajoelina wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ikulu ya rais huko Antananarivo, Aprili 29, 2019.
Rais wa Madagascar Andry Rajoelina wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ikulu ya rais huko Antananarivo, Aprili 29, 2019. Mamyrael / AFP
Matangazo ya kibiashara

Madagascar ambayo imerekodi visa 13, 086 vya maambukizi ya Corona baada ya visa vipya 214 kuthibitishwa katika muda wa saa 24 zilizopiota inaendelea kuathirika kiutoka na janga hilo. Kufikia sasa wagonjwa 10 816 wamepona ugonjwa huo hatari.

Siku ya Jumamosi hali ya dharura ilitangwa kwa siku 15.

Rais Andry Rajoelina ametangaza hatua zingine za kiafya ambazo raia watalazimika kufuata kwa wiki mbili zijazo. Hatua hizi ni zimelegezwa. Wakazi wa mji mkuu, Antananarivo, ambao walirudi kuwekwa tena kizuizini mwezi mmoja uliopita, wataweza kuendelea tena na maisha yao ya kila siku hatua kwa hatua.

Shughuli za kawaida zimerejeshwa tena na masoko yamefunguliwa tena hadi saa kumi na moja jioni katika mji mkuu wa Antananarivo pekee. Lakini usafiri wa umma umepigwa marufuku pamoja na kusafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

Analamanga, moja ya maeneo ya mji mkuu liko katika hatua ya "utulivu" kwa idadi ya visa vya maambukizi ya virusi vya Covid-19 kulingana na rais Andry Rajoelina, ambaye amesema kwamba amesikia kilio cha wakazi wa mji huo kutokana na hali ya kiuchumi inayowakabili.

Hakuna tarehe ya kufungua mipaka iliyotangazwa, isipokuwa huko Nosy Be, kaskazini-magharibi mwa nchi, moja ya visiwa vinavyotembelewa zaidi na watalii nchini Madagascar.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.