Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-CORONA-AFYA

Waziri Mkuu atangaza hatua mpya dhidi ya Covid-19 nchini Madagascar

Waziri Mkuu wa Madagascar Christian Ntsay metangaza kwenye runinga hatua zinazopaswa kutekelezwa ili kuendelea na vita dhidi ya ugonjwa hatari wa Covid-19.

Waziri Mkuu Christian Ntsay mwaka 2018.
Waziri Mkuu Christian Ntsay mwaka 2018. RFI / Sarah Tétaud
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumamosi jioni, baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri, serikali ilitangaza kusogeza mbele muda wa hali ya dharura ya afya kwa siku kumi na tano.

Madagascar imerekedi visa 2,078 vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo 18. Wiki hii, nchi hii, ambayo hivi karibuni ililegeza masharti ya kukabiliana dhidi ya ugonjwa huo hatari, ilijikuta idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona imeongezeka, hasa katika mji mkuu wa Antananarivo.

Ongezeko la idadi ya visa vya maambukizi "lilikuwa linatarajiwa", amebaini Waziri Mkuu Christian Ntsay, baada ya awamu ya kwanza ya kulegeza masharti ya kukabiliana na Corona kuanza kutumika miezi miwili iliyopita.

Hata hivyo Christian Ntsay anatambua kwamba watu wengi wa Madagascar hawajui wapi pa kwenda wakati wana shaka kuhusu hali yao ya afya na kwamba mchakato wa upimaji unachukua muda mrefu sana.

Wakati huo huo serikali ya Madagascar imesema kituo cha mapokezi na uchunguzi kitafunguliwa kila siku, saa 24 kwa siku, kuanzia Jumatano katika mji mkuu Antananarivo, kwa wakazi ambao wana dalili za virusi vya Covid-19.

Kulazwa kwa watu walipimwa virusi vya Corona sio lazima tena, Waziri Mkuu amebainisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.