Pata taarifa kuu
MADAGASCAR

Kifo cha rais Didier Ratsiraka: Madagascar yatangaza maombolezo ya kitaifa

Madagascar imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku moja  kufuatia kifo cha rais wa zamani Didier Ratsiraka aliyefariki jana Jumapili akiwa na umri wa miaka 84 katika hospitali ya jeshi ya Antananarivo.

Rais wa zamani Didier Ratsiraka alifariki Jumapili Machi 28, 2021 (Picha ya kumbukumbu).
Rais wa zamani Didier Ratsiraka alifariki Jumapili Machi 28, 2021 (Picha ya kumbukumbu). Rijasolo AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Ndugu zake wanabaini kwamba aliiga dunia kutokana na mshtuko wa moyo wakati alikuwa amelazwa hospitalini tangu Jumanne kwa "matibabu ya kawaida baada ya kupata homa ndogo". Viongozi mbalimbali duniani wametoa rambi rambi kwa taifa hilo na familia yake.

Rais wa sasa wa Madagascar, ambaye alikuwa alitoa rambi rambi zake kwa familia ya rais huyo wa kihistoria wa Madagascar Jumapili asubuhi kwenye ukurasa wake wa Facebook, alionekana mchana kwenye runinga ya taifa akitoa tena rambi rambi zake kwa familia.

Alikuwa kiongozi mahiri katika maisha ya kisiasa. Alikuwa Waziri wa Mambo ya nje wakati wa utawala wa Jenerali Ramanantsoa na alikuwa mmoja wa mawaziri vijana wakati huo. Kile watu wa Madagascar walipenda kutoka kwake ni wakati alijadili tena mkataba wa ushirikiano kati ya Madagascar na Ufaransa mnamo mwaka 1973. Wakati alikuwa Rais wa Jamhuri, alibeba na kuweka mbele maadili na utamaduni wa Madagascar. Umaarufu wake na na mtazamo wake ulielekezwa katika Bahari ya Hindi, Afrika na ulimwenguni kote. Bila kujali vyama vya kisiasa na tofauti za maoni, kila mtu anakiri kwamba amefanya mengi kwa nchi hii.

Alikataa ukoloni mamboleo na aliongoza sera ya nje kabisa, ambayo ni kusema kwa nchi za Magharibi na pia alifungua mlango wa Madagascar kwa nchi za Mashariki.

Marais wa zamani wapongeza kazi aliyoifanya Didier Ratsiraka

Aliyekuwa mkuu wa nchi Marc Ravalomanana, mpinzani mkubwa wa Didier Ratsiraka katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2001, alielezea "kusikitishwa kwake na huzuni yake baada ya kupata taarifa ya kifo cha rais huyo wa zamani. Hery Rajaonarimampianina, rais anayemaliza muda wake, amesema Didier Ratsiraka alikuwa mzalendo na mtu ambaye alifanya kazi kwa upatanisho wa kitaifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.