Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-USALAMA

Madagascar: Ishirini waangamia na wengine watoroka katika jela la Farafangana

Makabiliano kati ya wafungwa na walinzi wa jela katika jela la Farafangana, mji ulio kwenye pwani ya Kusini-Mashariki mwa Madagascar yamesababisha vifo kadhaa na majeruhi.

Nchini Madagascar, zaidi ya nusu ya wafungwa wamezuiliwa jela, wakisubiri kushtakiwa.
Nchini Madagascar, zaidi ya nusu ya wafungwa wamezuiliwa jela, wakisubiri kushtakiwa. Laetitia BEZAIN
Matangazo ya kibiashara

Vyanzo vya usalama vinabaini kwamba wafungwa waliasi dhidi ya walinzi wa jela hilo, linalopatikana katikati ya jiji na ambalo lina uwezo wa kupokea wafungwa 357.

Wafungwa 88 wametoroka, ikiwani pamoja na 20 ambao waliuawa. Wafungwa 39 hatimaye walipatikana baada ya polisi kuendesha msako katika mitaa mbalimbali. Wafungwa wengine zaidi ya ishirini bado wanatafutwa.

Kulingana na mashahidi, baada ya chakula cha mchana, wafungwa wa jela la Farafangana wamewashambulia walinzi wa gereza, baada ya dakika chache kikosi cha walinzi wa jela hilo wakajibu kwa rusha risasi. "Wafungwa walikuwa wengi na wengine walifanikiwa kuchukuwa bunduki kutoka kwa mmoja wa walinzi," Mkuu wa usalama, Jenerali Richard Ravalomanana amesema.

Mlinzi mmoja alijeruhiwa. Jela hilo lina wafanyakazi 44, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa ofisi na makarani, kwa jumala ya wafungwa 357.

"Uasi huo ulipangwa, kulingana na mkurugenzi wa magereza katika jimbo laAtsimo Atsinanana, Nadège Patricia Razafindrakala.

Picha za wafungwa waliouawa na wengine walioitoroka zilikuwa zikizunguka kwenye mitandao ya kijamii, hususan mtandao wa Facebook kwa siku ya jana hadi leo Jumatatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.