Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-CORONA-AFYA

Madagascar yaendelea kurekodi visa zaidi vya maambukizi

Visa vya maambukizi ya virusi vya Corona vinaendelea kuongezeka nchini Madagascar, nchi ambayo miezi kadhaa iliyopita rais Andry Rajoelina alitangaza kupata dawa inayoweza kuzuia na kuponya maambukizi hayo, ambayo kwa sasa yamefikia zaidi ya Elfu 13 na vifo vya watu karibu 150.

Serikali nchini Madascar inasema ongezeko la maambukizi hayo ni kwa sababu ya upimaji wa watu wengi unaoendelea, lakini pia maambukizi mengi ni katika jiji kuu Antananarivo, ambalo lina msongamano wa watu.
Serikali nchini Madascar inasema ongezeko la maambukizi hayo ni kwa sababu ya upimaji wa watu wengi unaoendelea, lakini pia maambukizi mengi ni katika jiji kuu Antananarivo, ambalo lina msongamano wa watu. RIJASOLO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema hospitali jijini Antananarivo, zinaelemewa na wagonjwa wa Covid-19, huku magari ya kuwabeba wagojwa yakionekana katika mitaa mbalimbali, na sasa uwanja wa michezo katika jiji hilo umegeuzwa kuwa hospitali ya muda, inayowapokea wagonjwa 250.

Wizara ya afya nchini humo imekuwa ikitangaza visa vipya kati ya 300 na 400 kila siku katika siku za hivi karibuni, takwimu zinazozua wasiwasi wa kuendelea kuongezeka kwa visa vya maambukizi hayo.

Serikali nchini humo inasema ongezeko la maambukizi hayo ni kwa sababu ya upimaji wa watu wengi unaoendelea, lakini pia maambukizi mengi ni katika jiji kuu Antananarivo, ambalo lina msongamano wa watu.

Aidha, serikali nchini humo inasema watu wanaoambukizwa hawakunywa dawa ya kiasilli iliyotangazwa na rais Rajoelina kama tiba ya maambukizi hayo, tiba ambayo wanasayansi wameonya kuwa haisaidii.

Hivi karibuni, kupitia barua aliyoandika kwa wafadhili wa kimataifa, Waziri wa afya alionya kushuhudiwa kwa maambukizi makubwa ya virusi hivyo, hasa jijini Antananarivo na kuomba msaada wa vifaa mbalimbali vya kusaidia kupambana  na janga hilo, huku serikali nchini humo ikisema hatua ya waziri huyo ilikuwa ya kibinafsi na hakumshirikisha rais Rajoelina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.