Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-COVID 19

Vyama vya kiraia vyatoa wito kwa mamlaka kuhusu chanjo

Idadi ya visa vya maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 inaendelea kuongezeka nchini Madagascar.

Kirusi cha Corona
Kirusi cha Corona NIAID-RML via AP
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na hali hiyo inayojirejea mara kwa mara nchini Madgascar tangu mwishoni mwa mwezi Desemba, vyama vya kiraia vimeitolea wito serikali kuwajibika: ni kwa sababu gani nchi hii bado inakataa kujiunga na mpango wa kimataifa wa chanjo ya bure? Kwa nini hakukuwa na mashauriano?

Nchini Madagascar, raia wengi wanaonekana hawajui kabisa juu ya uwepo wa chanjo iliyotengenezwa kupambana dhidi ya janga hili.

“Sina taarifa yoyote kama kweli kuna chanjo dhidi ya Covid! Hapa ndipo ninapata taarifa hiyo! Ndio, nimeshangazwa kwa kweli! ", amesema mmoja wa raia wa Madagascar akihojiwa na mwandishi wetu.

Wengi nchini humo wamebaini kwamba iwapo chanjo dhidi ya COVID-19 itaanza kutolewa, hawatosita kushiriki zoezi hilo.

Madagascar ni moja wapo ya nchi 92 zinazoendelea ambazo zimependekezwa kushiriki katika mpango wa "Covax Facility", mpango huu wa dunia wa kupata dozi ya chanjo dhidi ya COVID-19. Walakini, mwishoni mwa Novemba mwaka jana, msemaji wa serikali alitangaza kwamba Madagascar haitajiandikisha kwenye orodha ya nchi zinazonufaika.

Wakati huo msemaji wa serikali alithibitisha utayari wa nchi hiyo kuzingatia dawa zilizotengenezwa kienyeji, kama Covid-Organics, dawa ya asili ya mitishamba iliyotangazwa na rais, badala ya chanjo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.