Pata taarifa kuu

Kimbunga Emnati chatua Madagascar

Kimbunga Emnati kimetua nchini Madagascar usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano , nchi ambayo tayari imekumbwa na dhoruba kadhaa za kitropiki na kimbunga kwa mwezi mmoja, mamlaka Madagascar imesema.

Uharibifu uliosababishwa na kimbunga Batsirai huko MananjaryFebruari 7? 2022. Madagascar.
Uharibifu uliosababishwa na kimbunga Batsirai huko MananjaryFebruari 7? 2022. Madagascar. © Alkis Konstantinidis, Reuters
Matangazo ya kibiashara

"Kimbunga hicho kilitua mwendo wa saa kumi na moja kaskazini kidogo mwa wilaya ya Manakara" (kusini mashariki), Faly Aritiana Fabien, kutoka Ofisi ya Kitaifa ya Kudhibiti majanga (BNGRC), ameliambia shirika la habari la AFP.

Hali ambayo ilipitia Mauritius na Reunion katika Bahari ya Hindi, imepuza kasi baada ya kufika katika pwani ya mashariki mwa Madagascar, na upepo wa wastani wa kilomita 100 unaokwenda kwa saa moja na upepo wa kilomita 140 kwa unaokwenda saa moja .

Taarifa ya hivi punde ya mamlaka ya utabiri wa Hewa nchini Madagascar inaonya kuhusu mvua kubwa na hatari ya mafuriko na bahari kubwa katika ukanda wa kusini na kusini-mashariki. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yalisema siku moja kabla ya kujitayarisha "kwa mabaya zaidi".

Mapema Februari, Kimbunga Batsirai kiliua takriban watu 121, kuharibu maelfu ya nyumba na kuharibu mazao. Maelfu ya watu bado hawana makao. Mnamo Januari, Dhoruba ya Tropiki Ana tayari iliua takriban watu 100 nchini Madagascar, Msumbiji, Malawi na Zimbabwe.

Emnati alikuwa anaelekea kusini-magharibi asubuhi. Kulingana na utabiri, kimbunga hicho kinapaswa kuondoka kisiwani humo kupitia Idhaa ya Msumbiji usiku kucha kuanzia Jumatano hadi Alhamisi.

Zaidi ya watu 30,600 wamewekwa katika vituo vya malazi ya dharura kama tahadhari.

Moja ya nchi masikini zaidi duniani, Madagascar imekumbwa na ukame uliokithiri kwa miezi kadhaa katika eneo kubwa la Kusini, unaosababisha utapiamlo mkali na mifuko ya njaa.

Karibu dhoruba au vimbunga kumi huvuka Bahari ya Hindi kusini-magharibi kila mwaka wakati wa msimu wa vimbunga, ambao huanza mwezi wa Novemba hadi mwezi wa Aprili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.