Pata taarifa kuu

Wanamgambo washambulia Butembo baada ya MONUSCO kuondoka

Jeshi la Kongo limelipiza kisasi, na kuwaua washambuliaji wawili na kuwakamata wengine wanne. Mji wa Butembo unaopatikana katika mkoa w Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC umelengwa na shambulio siku ya Jumanne wiki hii, baada ya kundi la watu waliojihalmi kwa bunduki kuvamia mji huo, siku chache baada ya maandamano ya kupinga Umoja wa Mataifa mwishoni mwa mwezi Julai. 

Kulingana na Umoja wa Mataifa, MONUSCO itarejea Butembo "mara tu masharti ya kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wake yatakuwa yamezingatiwa".
Kulingana na Umoja wa Mataifa, MONUSCO itarejea Butembo "mara tu masharti ya kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wake yatakuwa yamezingatiwa". ©MONUSCO
Matangazo ya kibiashara

Wanamgambo wameshambulia eneo la kikosi cha Umoja wa Mataifa ambacho wafanyakazi wake walikuwa wametumwa nje ya jiji, kulingana na vyanzo kutoka mamlaka.

Jeshi limejibu masambulizii, washambuliaji wawili wameuawa na wanne kukamatwa, Kamishna Roger Mowa, meya wa mji wa Butembo, kituo kikuu cha kibiashara katika jimbo la Kivu Kaskazini, amewaambia waandishi wa habari. Jiji hilo, amehakikisha, liko "salama". Watu hawa wenye silaha "waliamini kwamba tulisema uwongo, kwamba Walinda amani wa MONUSCO (kikosi cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) hakijaondoka. Walikwenda kushambulia kituo hiki na kwa bahati nzuri, hawakupata kitu chochote ndani yake, ameongeza Meya.

Siku ya Alhamisi, gavana wa mkoa wa Kivu Kaskazini, ambaye alizuru mji wa Butembo, alihakikisha kwamba MONUSCO "tayari iliondoka" na kwamba vifaa vyake ambavyo bado viko mjini vitahamishwa. Hata hivyo MONUSCO ilihakikisha kwamba "haitaondoka Butembo" lakini " imesitisha shughuli zake kwa muda".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.