Pata taarifa kuu

DRC: Mamlaka yapaza sauti dhidi ya MONUSCO

Viongozi wa DRC wameongeza vikao baada ya matukio ya usalama na maandamano dhidi ya MONUSCO, tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC. Maandamano yalifanyika usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne yakimlenga Felix Tshisekedi. Marais wa mabaraza mawili ya Bunge, Waziri Mkuu na mawaziri wachache walihusishwa kutathmini hali hiyo.

Rais wa DRC Felix Tshisekedi.
Rais wa DRC Felix Tshisekedi. Sumy Sadurni / AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Wakati wa mkutano wa baraza la mawaziri Ijumaa ya wiki iliyopita, rais Felix Tshisekedi aliitaka MONUSCO kuanza kuondoa askari wake hatua kwa hatua. 

Kupitia taarifa, serikali imeagiza kufanyika mkutano na MONUSCO ili kujadili juu ya mpango wake wa kuondoka nchini humo, bila ya kufafanua zaidi.

Serikali ya Kongo imesema raia 29 na wanajeshi wanne wa MONUSCO waliuawa wakati wa maandamano yaliyotokea mashariki mwa nchi hiyo. 

Waandamanaji walikuwa wanashinikiza askari hao kuondoka nchini humo kwa kushindwa kuwalinda raia dhidi ya mashambulizi kutoka makundi ya waasi ambayo yamesababisha uharibifu mkubwa katika eneo hilo kwa miongo kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.