Pata taarifa kuu

DRC: Marekani inataka mamlaka nchini humo kuwalinda wafanyikazi wa UN

Marekani imetoa wito kwa mamlaka nchini Jamuhuri  ya kidemokrasia ya Kongo kuhakikisha wafanyikazi wa umoja mataifa nchini humo wanalindwa pamoja na afisi zao.

Maandamano dhidi ya Monusco,mjini Goma DRC  Julai 26 2022.
Maandamano dhidi ya Monusco,mjini Goma DRC Julai 26 2022. AFP - MICHEL LUNANGA
Matangazo ya kibiashara

Wito wa Marekani umekuja baada ya walinda usalama wa UN katika taifa hilo la Afrika ya kati kuawaua katika maandamano ya kupinga uwepo wao nchini DRC wiki hii.

Karibia raia 12 waliripotiwa kuawaua nchini DRC siku ya Jumanne katika maandamano dhidi ya walinda usalama wa MONUSCO, ambao wanatuhumiwa na raia kwa kufeli kuwalinda kutokana na mashambulio ya makundi ya waasi.

Mwanajeshi mmoja wa umoja wa mataifa na maofisa wawili wa polisi wa umoja huo waliripotiwa kuawaua katika makabiliano kati ya waaandamanaji na walinda usalama.

Waandamanaji walishambulia kambi za umoja wa mataifa katika miji minne katika majimbo ya Kivu kaskazini na Kivu kusini.

Walinda usalama wa UN kwa upande wao wamekana madai kuwa walifyatua risasi za moto kuelekea walikokuwa waandamanaji.

Licha ya walinda usalama kuwa DRC kwa miaka 22, waasi waendelea kutekeleza mashambulio na mauwaji ya raia mashariki mwa taifa hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.