Pata taarifa kuu

Viongozi wa SADC wakutana kujadili masuala mbalimbali katika nchi zao

Viongozi kutoka Jumuiya ya kiuchumi ya  nchi za Kusini mwa Afrika SADC wanakutana leo na kesho jijini Kinshasa, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kujadili masuala mbalimbali. 

Mkutano wa SADC juu ya hali ya uchaguzi nchini DRC Desemba 2018 (picha ya zamani).
Mkutano wa SADC juu ya hali ya uchaguzi nchini DRC Desemba 2018 (picha ya zamani). Reuters/Bouka Roch
Matangazo ya kibiashara

Wakuu wa nchi wanaokutana kwenye mkutano huu wa 42, wanajadiliana kuhusu namna ya kuimarisha ukuaji wa viwanda, kilimo na masuala ya madini katika nchi hizo. 

Mbali na masuala ya kiuchumi, DRC ambayo ni mwenyeji wa mkutano huu, inatarajiwa kutumia mkutano huu kutafuta msaada wa kurejesha amani katika eneo la Mashariki ambalo limeendelea kukumbwa na utovu wa usalama. 

Mkutano mkuu hufanyika kila mwaka, kuwaleta pamoja, viongozi kutoka nchi 16 kujadili, masuala mbalimbali yanayoikumba Jumuiya hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.