Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-USALAMA

Serikali ya Kongo inautaka Umoja wa Mataifa kumfukuza msemaji wake nchini DRC

Baada ya kuomba kutathminiwa upya kwa ratiba ya kujiondoa hatua kwa hatua kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa, serikali ya Kongo imeomba rasmi kuondoka kwa msemaji wa MONUSCO Mathias Gillmann, ambaye inamtuhumu, katika mahojiano na RFI, kwa kuchochea hali ya wasiwasi inayoendelea nchini humo. Barua rasmi imetumwa kwa MONUSCO ili kuonyesha msimamo wa mamlaka ya DRC.

Mlinda amani wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) akiwa ameketi kwenye helikopta juu ya ghala la kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko Goma, katika mkoa wa Kivu Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, tarehe 26 Julai 2022.
Mlinda amani wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) akiwa ameketi kwenye helikopta juu ya ghala la kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko Goma, katika mkoa wa Kivu Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, tarehe 26 Julai 2022. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na serikali ya Kongo, mvutano uliopo kati ya raia na MONUSCO unatokana hasa na kauli zinazochukuliwa kuwa "zisizo na hisia na zisizofaa" za Mathias Gillmann. Katika mahojiano na RFI mnamo Julai 13 huko Kinshasa, msemaji wa MONUSCO alisema kuwa kupelekwa kwa sehemu kubwa ya wanajeshi wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa na jeshi la Kongo katika mapambano dhidi ya kundi la waasi la M23 kutakuwa na matokeo mabaya. Akirejelea maneno ya Bintou Keita, mkuu wa MONUSCO katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, pia alieleza kuwa kundi la M23 linajiendesha kama jeshi halali lenye silaha za kijeshi za hali ya juu.

Katika wiki za hivi karibuni, MONUSCO ilisisitiza juu ya uharaka wa kufikia makubaliano ya kusiishwa kwa mzozo huu unaohusisha M23 ili kwamba ujumbe huo na jeshi la DRC, FARDC,  wakabiliane na mizozo mingine.

Katika barua iliyotumwa kwa Bintou Keita, Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC, Christophe Lutundula, anaona kuwa "uwepo wa Mathias Gillmann hauwezi kukuza hali ya uaminifu na utulivu kati ya taasisi za DRC na MONUSCO, kukamilisha mpango wenye madhumuni ya kujiondoa kwake moja kwa moja kutoka DRC”.

Kwa upande wa MONUSCO, wanasema wanashangazwa kuibka kwa mzozo huu na kuficha "matatizo halisi".

Wakati huo huo, katika katika mapambano, waasi wa kundi la M23 walianza tena mashambulizi yao na waliwasili jana katika eneo linalopatikana kwenye umbali wa takriban kilomita thelathini kutoka Goma, karibu na kambi ya kijeshi ya Rumangabo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.