Pata taarifa kuu
USALAMA-UGAIDI

Ayman al-Zawahiri, mhusika mkuu katika jihadi ya Kiislamu barani Afrika

Alikuwa mmoja wa magaidi waliokuwa wakitafutwa sana duniani. Ayman al-Zawahiri, kiongozi wa al-Qaeda, aliuawa mwishoni mwa juma hili lililopita na shambulio la ndege zisizo na rubani za Marekani kwenye ghorofa moja mjini Kabul. Habari hiyo imethibitishwa na Joe Biden.

Kiongozi al-Qaeda, raia wa Misri, Ayman al-Zawahiri, aliuawa katika shambulio la ndege isiyo na rubani ya Marekani iliyomlenga mjini Kabul.
Kiongozi al-Qaeda, raia wa Misri, Ayman al-Zawahiri, aliuawa katika shambulio la ndege isiyo na rubani ya Marekani iliyomlenga mjini Kabul. © SITE Monitoring Service/Handout via REUTERS TV
Matangazo ya kibiashara

Al-Zawahiri alijulikana sana kuliko jina la bin Laden, labda hata zaidi katika bara la Afrika. Kwa sababu daktari huyu wa upasuaji kutoka Misri alikuwa amezindua harakati zake zote duniani na Afrika kupitia makundi mbalimbali. Moja ya muhimu zaidi kati ya makundi hayo ni AQIM, al-Qaeda katika eneo la Maghreb.

Tayari mwaka 2002, aliweka hatua za kwanza za mkakati wa al-Qaeda barani Afrika. Kundi hilo lilikuwa limetekeleza mashambulizi ya kwanza katika bara hilo miaka minne iliyopita, likilenga balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania. Lakini hadi mwezi Januari 2007 ambapo al-Qaeda katika eneo la Maghreb  lilianzishwa. AQIM ilichukua nafasi kutoka kwa kundi la GSPC kutoka Algeria, kundi la Salafi linalojihusisha na kuhubiri na kupambana. Makubaliano hayo yalitiwa saini na Ayman al-Zawahiri na Abdelmalek Droukdel. Abdelmalek Droukdel, kiongozi wa kjihadi kutoka Algeria, aliendeleza kundi la AQIM kwa kupanua ushawishi wake katika ukanda wa Sahel. 

Baada ya wanajihadi kuchukua eneo la kaskazini mwa Mali mwaka 2012, kisha kuingilia kati kwa jeshi la Ufaransa, AQIM ilipoteza mwelekeo. Lakini kundi hili lilipata ushawishi tena kutoka mwaka 2017 wakati kundi jipya lilipoundwa: Kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu (Jnim, kifupi chake kwa Kiarabu). kundi hili jipya lilileta pamoja makundi kadhaa ya wanajihadi: AQIM, Ansar Dine, Ansarul Islam, Katiba Serma na Katiba Macina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.