Pata taarifa kuu

Patrice Lumumba: Miaka 61 baada ya kifo chake, Ubelgiji yarejesha mabaki yake kwa familia

Mnamo Januari 17, 1961, Waziri Mkuu wa Kongo Patrice Emery Lumumba aliuawa huko Katanga akiwa na wanaharakati wenzake wawili Joseph Okito na Maurice Mpolo. Jino moja tu lilipatikana nchini Ubelgiji miaka kadhaa baadaye. Na ni "salio" hili litakalokabidhiwa kwa familia yake wakati wa sherehe katika Jumba la Edgemont huko Brussels, Jumatatu hii, Juni 20, 2022.

Waziri Mkuu wa Kongo Patrice Lumumba akisalimiana na umati wa wafuasi wake wakati akiondoka kwenye ukumbi wa jengo la utamaduni huko Léopoldville mnamo Agosti 27, 1960.
Waziri Mkuu wa Kongo Patrice Lumumba akisalimiana na umati wa wafuasi wake wakati akiondoka kwenye ukumbi wa jengo la utamaduni huko Léopoldville mnamo Agosti 27, 1960. AP
Matangazo ya kibiashara

"Roho yake itaweza kupumzika kwa amani", amesema Roland Lumumba, mmoja wa watoto wa Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Kongo aliyeuawa. Yeye na ndugu zake watapokelewa na Mfalme wa Ubelgiji kabla ya sherehe. Hii itakuwa mwisho wa mapambano ya muda mrefu ambayo yatakuwa yamedumu zaidi ya miaka 60 na hatimaye kuweza kuzika na kutoa heshima ya mwisho kwa baba, mwanasiasa, lakini pia kwa yule ambaye bado anadhihirisha uhuru wa Kongo hadi leo.

Kwa muda mrefu, familia na raia wengi nchini DRC walidhani kwamba hakuna kilichobaki kwa baba huyo wa taifa. Mwili wake pamoja na ile ya wenzake wawili, Joseph Okito na Maurice Mpolo, iliyeyushwa kwa tindikali baada ya vifo vyao. Lakini miaka kadhaa baadaye, mnamo 2016, jino la mtetei huyu wa uhuru wa Kongo lilikamatwa na mahakama katika kesi ya mmoja wa maafisa wa Ubelgiji, Gérard Soete, aliyehusika na kuficha ukweli kuhusu mauaji ya shujaa wa kitaifa.

Hata hivyo jino hilo lilithibitishwa kuwa ni la Patrice Lumumba. Hakika, miaka michache mapema, Gérard Soete alijisifu, mbele ya wanahabari wa televisheni, kwamba ana"ukumbusho" wa usiku huo wa kutisha.

 Ni jino hili ambalo mahakama ya Ubelgiji yatakabidhi familia yake wakati wa sherehe itakayofanyika katika hatua mbili katika Jumba la Egmont Jumatatu hii. Likiwa kwenye sanduku, litawekwa kwenye jeneza kabla ya hotuba ya mkuu wa serikali ya Ubelgiji, Alexander De Croo.

Kisha mwili huo utakwenda kwa Ubalozi wa DRC mjini Brussels ambako kwa kurudishwa katika ardhi ya Kongo utakaribishwa na Waziri Mkuu Jean-Michel Sama Lukonde. Rais Tshisekedi akiwa amefuta safari yake, huku nchi hiyo ikikumbwa na mzozo mkubwa wa usalama katika eneo la Mashariki. Raia watakuwa na saa 24 za kutoa heshima zao.

Baada ya Ubelgiji, mabaki ya Patrice Lumumba yatasafiri kwa ndege hadi DRC Jumanne jioni. Hatua ya kwanza katika kijiji chake cha asili, Onalua mji ambao umebadilishwa jina na kuitwa Lumumba-ville, huko Sankuru. Kisha litasafirishwa hadi Kinsangani, mahali ambapo alianzisha chama chake, Kongo National Movement. Na hatimaye, litasafirishwa hadi Shilatembo, karibu na Lubumbashi, huko Katanga, alikouawa.

Mbunge wa Ubelgiji, Kalvin Soiresse Njall, amesema zoezi la kukabidhiwa kwa mabaki ya Patrice Lumumba ni la kihistoria hata kama limechelewa sana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.