Pata taarifa kuu
ETHIOPIA

Waasi wa Tigray wapambana na wanajeshi wa Eritrea

Nchini Ethiopia, waasi wa Tigray wameripotiwa kukabiliana vikali na wanajeshi wa Eritrea, katika jimbo la Tigray, yakiwa ndio mapigano makubwa kutokea baada ya kuripotiwa kwa usitishwaji wa vita mwezi Machi.

Waasi wa Tigray nchini Ethiopia
Waasi wa Tigray nchini Ethiopia © Finbarr O'Reilly / The New York Times
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema mapigano hayo yalitokea Mei 24, huku waasi wa Tigray wakisema walifanikiwa kuwasambaratisha wanajeshi hao wa Eritrea.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Getachew Reda mshauri wa rais wa jimbo la Tigray amesema, mapigano hayo yalisababisha maafa makubwa kwa upande wanajeshi wa Eritrea waliokuwa wamevuka mpaka na kuja kuwashambulia.

Inaelezwa kuwa makabiliano hayo yalitokea katika milima ya Geza na Gille, katika barabara ya kuelekea mjini Badme, na waasi wa Tigray wanasema waliuwa wanajeshi 120 wa Eritrea na kuwajeruhi wengine 195.

Eritrea haijasema chochote kuhusu ripoti ya kuwepo kwa mapigano hayo, lakini ni kawaida kwa rais Issayas Afewerki kuagiza operesheni ya kijeshi kila tarehe 24 Mei, siku ambayo nchi hiyo ilitangaza uhuru na kujitenga na Ethioia mwaka 1991.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.