Pata taarifa kuu
Ethiopia Usalama

Benki ya dunia kushirikiana na Ethiopia

Benki ya dunia itaipa serikali ya Ethiopia kima cha shilling dolla millioni 300, zitakazotumika kusaidia kujenga upya maeneo yalioharibiwa kutokana na vita hasa katika jimbo la Tigray, wizara ya fedha ya Ethiopia imesema.

sehemu ya jengo la Benki ya dunia
sehemu ya jengo la Benki ya dunia © Wikimedia Commons CC-BY-SA 3.0 Victorgrigas
Matangazo ya kibiashara

Kwa mjibu wa serikali ya Ethiopia, pesa hizo pia zitatumika kutoa huduma za jamii katika maeneo yalioathirika, baadhi ya huduma hizo zikiwa matibabu, elimu, usambazaji wa maji na kusaidia walioathirika na dhuluma za kijinsia.

Maeneo yatakayonufaika na pesa hizo ni Tigray, Amhara, Afar, Oromia na Benishangul Gumuz, serikali ikisema itashirikiana na mashirika mengine kuhakikisha hilo linatekelezwa.

Vita vya Oromia na Benishangul Gumuz ni tofauti na vile vya jimbo la Tigray.

Mapigano yalizuka jimboni Tigray mwaka 2020, na kusambaa katika majimbo jirani ya Afar na Amhara mwaka uliopita, ila kwa sasa yamesitishwa ili kutoa misaada kwa walioathirika

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.