Pata taarifa kuu

UN, inataka uchunguzu huru kufanyika kuhusiana na machafuko ya kidini nchini Ethiopia.

Mkuu wa tume ya haki za binadamu katika umoja wa mataifa UN, Michelle Bachelet, amekashifu machafuko ya kidini ya hivi punde kati ya waumini wa dini ya kikristo wa waisilamu nchini Ethiopia , akitoa wito wa uchunguzi huru na wa kina kufanyika kwa haraka kubaini chanzo za matukio hayo.

Michelle Bachelet, mjumbe wa umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu.
Michelle Bachelet, mjumbe wa umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu. AP - Martial Trezzini
Matangazo ya kibiashara

“Nimeghadhishwa sana na machafuko ya hivi punde kati ya waisilamu na wakristo wa dhehebu la Orthodox nchini Ethiopia ambapo karibia watu 30 waliripotiwa kuuwawa zaidi ya wengine 100 wakiaachwa na majeraha,” Imesema taarifa yake Michelle Bachelet.

Bachelet, ametoa wito kwa mamlaka nchini   Ethiopia kuruhusu kufanyika kwa uchunguzi wa wazi katika tukio hilo ili wahusika wakabiliwe kwa muijbu wa sheria.

Aidha mjumbe huyo wa UN, ametaka kuwepo kwa mazungumzo ya kupatanisha jamii zinazohasimiana kwenye taifa hilo lenye idadi ya raia milioni 115, theluthi tatu ya raia hao wakiwa ni waisilamu.

Makabiliano hayo ya hivi punde ya kidini yameripotiwa kutokea kwenye mji wa Gondar katika wilaya ya Amhara April 26, wakati wa shughuli ya mazishi ya kiisilamu kwenye ardhi inayozozaniwa kati ya wakristo na waisilamu.

 “Naelewa kuwa miskiti miwili iliteketezwa nyengine mbili ikiharibiwa katika eneo la Gondar. Kutokana na tukio hilo, waathiriwa walilipiza kisasa kwa kuchoma moto hadi kufa wanaume wawili waumini wa kanisa la Orthodox, mtu mwengine akauwawa kwa kukatwa kwa panga, makanisa tano yakachomwa katika eneo la Silt’e,” Mjumbe huyo wa UN ameeleza zaidi.

Taarifa zinaeleza kuwa tangu kutokea kwa machafuko hayo mwezi jana, mamlaka nchini Ethiopia imewakamata zaidi ya watu 570 kutoka miji minne.

Mamlaka jijini Addis Ababa, Jumatatu ya wiki iliyopita iliwakamata watu 76 wanaoshukiwa kuhusika na machafuko yaliotokea wakati wa sherehe za maombi ya Idd al –Fitr eneo ambalo maelfu ya waisilamu walikuwa wamekusanyika kwa shughuli za kumaliza mwezi mtukufu wa Ramadan.

“Wale waliokamatwa wanafaa kushtakiwa kwa mujibu wa kanuni na sheria za kimataifa kuhusu haki za binadamu bila ubaguzi wowote,” Amesisitiza Bachelet mjube wa UN.

Tangu mwaka wa 2019, machafuko ya kidini yamekuwa yakiripotiwa kwenye taifa hilo lati ya waisilamu na wakristo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.