Pata taarifa kuu

Mkutano wa COP15 umeanza jijini Abidjan nchini Cote Dvoire kujadili utunzaji misitu

Mkutano wa Kimataifa wa COP15, unaolenga kujadili mbinu mbalimbali za kuzuia shughuli za binadamu zinazochangia uharibifu wa misitu na  udongo umeanza jijini Abidjan nchini Cote Dvoire.

Mkutano wa COP15 jijini  Abidjan,Côte d’Ivoire.
Mkutano wa COP15 jijini Abidjan,Côte d’Ivoire. REUTERS - LUC GNAGO
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu wa 15 unawakutanisha viongozi mbalimbali wa dunia na watalaam mbalimbali, Jumatatu mpaka Mei 22, kujadili namna ya kuhakikisha kuwa misitu na ardhi yenye rotuba inalindwa dhidi ya shughuli za binadamu.

Mwenyeji wa mkutano huo, rais Alassane Ouattara ametaka hatua za haraka kuchukuliwa ili kuokoa bara la Afrika na dunia.

Kauli mbiu ya mkutano huu, ni ardhi, maisha na kuacha alama, kutoka ukosefu hadi mafanikio, kwa kuhakikisha kuwa, ardhi inaendelea kunufaisha kizazi cha sasa hivi na kile kinachokuja.

Mkutano huu unafanyika wakati huu ripoti ya Umoja wa Mataifa, ikieleza kuwa, asilimia 41 ya ardhi imeharibiwa, sawa na hekari Milioni 12, ukubwa wa nchi ya Benin au Ubelgiji.

Wajumbe wanatarajiwa kuja na mbinu kwa nchi wanachama kuhakikisha kuwa, ardhi na misitu inalindwa ili kuepusha ukame katika nchi mbalimbali za dunia, suala ambalo limesababisha ukame na kuleta madhara makubwa kama baa la njaa.

Bara la Afrika hupoteza msitu wa ukubwa wa ekari zaidi ya Milioni nne, kila mwaka, na inahofiwa kuwa kufikia mwaka 2030, uharibifu huo uitafikia hekari Milioni Sita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.