Pata taarifa kuu
CHAD-UCHUNGUZI

CHAD: Uchunguzi juu ya kifo cha Idriss Déby

Mwaka mmoja aas umepita tangu rais wa Idriss Déby afariki dunia katika mazingira ya kutatanisha, katikati mwa mashambulizi ya waasi wa FACT, nchini Chad, na Baraza la Mpito la kijeshi likaanzishwa. Siku chache kabla ya maadhimisho haya ya kwanza, RFI inakupa uchunguzi wa pamoja katika vipindi vinne kuhusu mazingira ya kifo cha rais wa Chad, na kuhusu hali ya kipindi cha mpito leo, kulingana na shuhuda nyingi.

Idriss Déby Itno katika mavazi yake ya Kimarshal, cheo cha ufahari alichopewa nchini Chad.
Idriss Déby Itno katika mavazi yake ya Kimarshal, cheo cha ufahari alichopewa nchini Chad. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Aprili 11, 2021, wakati wananchi wa Chad walialikwa kupiga kura ili kumpigia kura Idriss Déby na kumpa muhula wa 6 bila upinzani wowote, kundi la waasi la FACT lilitangaza kwamba linaanzisha mashambulizi... Lengo lake, kulingana na kiongozi wake Mahamat Mahdi Ali: kuvuruga kura, kukabiliana na askari, kuwezesha raia kupinga utawala... Kwa hili, alisema, ana kikosi maalumu cha wapiganaji 600 na wapiganaji 2,500 hadi 3,000 wenye silaha za kutosha.

Kwa kweli, wapiganaji wake walikuwa tayari wameondoka Libya tangu Aprili 6 ... Wakati huo huo walidhibiti eneo la Magharibi la Tibesti, wakagajigawa baadhi wakaelekea Faya Largeau wakati idadi kubwa ya wapiganaji walikwenda kusini, kwenye jangwa la Kanem, ili kupunguza hasara iliyosababishwa na mashambulizi ya anga. Katika eneo hili, waasi wa FACT iwalitarajia kupata msaada na vifaa...

Wanajeshi wa Chad na washirika wao Ufaransa walizidiwa nguvu... Siku ya Ijumaa, Aprili 16, akirejea kutoka safari nchini Congo-Brazzaville, Idriss Déby alifahamu jinsi waasi hao wanavyosonga mbele... Siku iliyofuata, dhidi ya ushauri wa makao makuu wa jeshi lake na familia yake, aliondoka na vitani... Kuwatia moyo wanajeshi wake ni tabia ya Marshal...

"kwa upande wake aliema kiongozi lazima awe pamoja na jeshi lake" alishuhudia mmoja wa washirika wake wakaribu wa zamani...

Jinsi waasi wa FACT walivyoendesha mashambulizi mwezi Aprili 2022.
Jinsi waasi wa FACT walivyoendesha mashambulizi mwezi Aprili 2022. © RFI

"Mwokozi mkubwa" kama alivyoitwa wakati mwingine huko N'Djamena, aliwakuta mtoto wake Mahamat, ambaye wakati huo alikuwa anaongoza kikosi cha ulinzi wa rais, na mkuu wa majeshi, Jenerali Daoud...

Mapigano hayo yaliyoanza Jumamosi tarehe 17 yaliendelea hadi Jumatatu tarehe 19...

Ilikuwa wakati wa moja ya mapigano hayo ambapo Idriss Déby aliuawa ...

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.