Pata taarifa kuu
CAR-MAZUNGUMZO

CAR: Mazungumzo ya maridhiano ya kitaifa yafunguliwa bila upinzani

Mazungumzo ya maridhiano ya kitaifa yaliyoahidiwa kwa muda mrefu na Rais Faustin Archange Touadéra nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, inayokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 2013, yamefunguliwa Jumatatu lakini bila makundi yenye silaha, ambayo hawajaalikwa, wala upinzani ambao umesusia, kulingana na mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP, liyehudhuria kikao hicho.

Jamhuri ya Afrika ya Kati: mazungumzo bila wahusika wakuu wa mgogoro.
Jamhuri ya Afrika ya Kati: mazungumzo bila wahusika wakuu wa mgogoro. © REUTERS - ANTOINE ROLLAND
Matangazo ya kibiashara

Siku sita zilizopita, Bw. Touadéra alitangaza kwamba "mazungumzo ya jamhuri" na upinzani na mashirika ya kiraia, ambayo alikuwa ameahidi miezi 15 iliyopita baada ya uchaguzi uliokuwa na upinzani mkali, yatafanyika Jumatatu, lakini mpango ambao haukuwa unaeleweka na bila kutaja malengo madhubuti mwishoni mwa mijadala iliyopangwa kudumu kwa wiki moja pekee.

Rais Touadera amefungua mazungumzo ya Jamhuri mbele ya mamia ya washiriki kutoka kwa walio wengi, mashirika ya kiraia na watu binafsi walioalikwa kwenye sherehe ya ufunguzi katika makao makuu ya Bunge. "Sote tumehamasishwa kuzungumzia amani (...) hakuna suala la mwiko, tuko hapa kusema kinaga ubaga kinachotusibu (...), kuondoa vizingiti kama familia", rais Touadera amesema, huku akizungukwa na raia wawili wa Urusi walio katika kikosi chake cha ulinzi, nyuso zao zikiwa zimefunikwa.

Siku ya Jumapili, takriban vyama vyote vya upinzani vilitangaza havitashiriki katika mazungumzo hayo hasa kwa sababu waasi hawajaalikwa na mpango huo haujumuishi chochote kuhusu kile inachokiita "swali la mgogoro wa baada ya uchaguzi" ni kusema kile inachochukulia kuwa kuchaguliwa tena kwa Bw. Touadéra mnamo Desemba 27, 2020 na ushiriki mdogo wa wapiga kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.