Pata taarifa kuu
CAR-USALAMA

CAR: Umoja wa Mataifa walaani vizuizi dhidi ya uchunguzi wa mauaji kadhaa

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati alimaliza ziara yake nchini humo siku ya Alhamisi. Wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akitia saini ripoti ya kutisha juu ya unyanyasaji unaofanywa kila upande, kutumia wanamgambo na kulenga baadhi ya watu kwa sababu ya makabila yao, Yao Agbetse amelani vizuzi kwa kazi ya Umoja wa Mataifa kuhusiana na uchunguzi.

Katika muda wa miezi minne, Umoja wa Mataifa umerodhesha takriban raia 229 waliouawa, umejunguza matukio manne ya mauaji na, kwa karibu nusu ya mauaji hayo, Umoja wa Mataifa unasema vikosi vya Jamhuri ya Afrika ya Kati (FACA) na washirika wao Urusi vinahusika.
Katika muda wa miezi minne, Umoja wa Mataifa umerodhesha takriban raia 229 waliouawa, umejunguza matukio manne ya mauaji na, kwa karibu nusu ya mauaji hayo, Umoja wa Mataifa unasema vikosi vya Jamhuri ya Afrika ya Kati (FACA) na washirika wao Urusi vinahusika. AFP PHOTO / FRED DUFOUR
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya nchi mbili vya Urusi na FACA vinanyooshewa kidole. Vizuizi ambavyo, kulingana na Yao Agbetse, vinatishia udhihirisho wa ukweli, hasa kuhusu mauaji kadhaa yaliyofanywa katika miezi ya hivi karibuni.

Katika muda wa miezi minne, Umoja wa Mataifa umerodhesha takriban raia 229 waliouawa, umejunguza matukio manne ya mauaji na, kwa karibu nusu ya mauaji hayo, Umoja wa Mataifa unasema vikosi vya Jamhuri ya Afrika ya Kati (FACA) na washirika wao Urusi vinahusika.

"Tumeambia mamlaka kwamba ni muhimu kuweka mstari mwekundu ambao washirika wake hawawezi kuuvuka," amesema Yao Agbetse, mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kwa sababu ni jambo moja kutoa usaidizi ili hali iweze kuimarika - na hilo lilithaminiwa - lakini jambo lingine ni kuweka vizuizi njiani, wakati mwingine kuzuia kazi ya wachunguzi. "

Wachunguzi waliozuia hasa kwenda kwenye maeneo ya migodi, kulikotokea mapigano makali, na ambapo raia wengi pia waliuawa. “Iwapo tutazuiwa kufika mahali ambapo visa vya ukiukaji viliripotiwa, hii inaweza kuainisha b kwamba vyombo vinavyoendelea kwa njia hii havitaki ukweli ujulikane na hili halikubaliki. "

Ripoti ya hivi punde pia ina wasiwasi kuhusu kuajiriwa kwa wanamgambo wa anti-balaka na Faca na washirika wao kutoka Urusi. Pamoja na kulenga mara kwa mara watu kutoka jamii za Fulani na Waislamu. Vikosi vinavyounga mkono serikali kwa sasa vinaendelea na mashambulizi yao kaskazini mashariki mwa nchi karibu na maeneo makuu ya uchimbaji madini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.