Pata taarifa kuu
CAR-USALAMA

Mkuu wa Umoja wa Mataifa apinga unyanyasaji unaofanywa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Katika ripoti yake ya hivi punde iliyowasilishwa mbele ya Baraza la Usalama, Antonio Guterres amevinyooshea kidole cha lawama vikosi vya usalama na jeshi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, pamoja na "washirika wao wa kigeni", akiwataja kwa neno hili mamluki wa kundi la Wagner.

Mwanajeshi wa shirika la Wagner, huko CAR.
Mwanajeshi wa shirika la Wagner, huko CAR. © Franceinfo
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti yake ya hivi punde, mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa anakaribisha usitishaji vita uliotangazwa tarehe 15 Oktoba na Rais Touadéra lakini anasikitishwa na kukosekana kwa maendeleo yanayoonekana tangu wakati huo. Kwa upande mmoja, mvutano wa kisiasa unaendelea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, mazungumzo ya kitaifa yamesimama, na hivyo kuweka ugumu makubaliano ya mwaka 2019.

Na ingawa visa vya ukiukwaji wa makubaliano ya amani vimepungua kwa 30% tangu ripoti yake ya mwisho, hali ya usalama bado ni tete, kulingana na Antonio Guterres. Kama ushahidi, visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilivyorodheshwa na tume ya Umoja wa Matiafa nchini humo, MINUSCA, havijapungua, na vinaendelea kumchukiza.

Pia amehimiza Bangui kudhibiti vyema vikosi vya Jamhuri ya Afrika ya Kati, pamoja na "maafisa wengine wa usalama" - hivi ndivyo alivyowaita wanamgambo wa shirika la Wagner kutoka Urusi. Amelaani operesheni kadhaa zilizofanywa na jeshi na mamluki hao, ikiwa ni pamoja na ile iliyosababisha vifo vya raia 17 mwezi uliopita karibu na mji wa Bria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.