Pata taarifa kuu
CAR-USALAMA

CAR: Operesheni ya Faca na washirika wao wa Urusi yazua sintofahamu

Raia kadhaa waliripotiwa kuuawa wakati wa operesheni ya pamoja ya kijeshi ya vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faca, na washirika wao wa Urusi. Operesheni iliyofanyika mapema wiki hii dhidi ya waasi wa CPC karibu na mji wa Bria, kilomita 600 mashariki mwa mji mkuu wa Afrika ya Kati Bangui.

Kulingana na vyanzo vya habari, operesheni ya pamoja ya Faca na washirika wao kutoka Urusi ilifanyika Jumapili na Jumatatu iliyopita huko Aigbando, eneo kunakochimbwa madini lililoko kilomita 75 kaskazini mwa Bria.
Kulingana na vyanzo vya habari, operesheni ya pamoja ya Faca na washirika wao kutoka Urusi ilifanyika Jumapili na Jumatatu iliyopita huko Aigbando, eneo kunakochimbwa madini lililoko kilomita 75 kaskazini mwa Bria. AFP
Matangazo ya kibiashara

Opereheni hii imeibua maswali mengi kwa sababu ya uwepo wa kikosi cha watu kutoka Urusi wakishirikiana na vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faca. Hivi karibuni Bangui ilitangaza kwamba watu kutoka Urusi ni  wakufunzi waliokuja kutoa mafunzo kwa jeshi lake. hata hivyo kulingana na vyanzo vya kutoka nchini humo, watu hao kutoka Urusi ni mamluki kutoka kundi la Wagner, ambalo linashutumiwa mara kwa mara na raia kwa unyanyasaji.

Kulingana na vyanzo vya habari, operesheni hiyo ya pamoja ilifanyika Jumapili na Jumatatu ya wiki iliyopita huko Aigbando, eneokunakochimbwa madini lililoko kilomita 75 kaskazini mwa Bria. Vikosi vya jeshi vya Jamhuri ya Afrika ya Kati - Faca - vikisaidiwa na kikosi cha watu kutoka Urusi vilianzisha mashambulizi dhidi ya kundi lenye silaha la muungano wa waasi wa CPC ambao linashikilia eneo hilo.

Kulingana na vyanzo kutoka nchini Jmhuri ya Afrika ya Kati, zaidi ya raia thelathini waliuawa. Baadhi waliuawa wakati wa operesheni hiyo ya kijeshi; wengine walipelekwa msituni na kisha kuuawa, kimeongeza chanzo hiki, kinachozubaini kwamba yalikuwa "mauaji". Wanawake na watoto wawili ni miongoni mwa watu waliouawa. "Tuna wasiwasi sana", kinaongeza chanzo hiki.

Huko Bria, chanzo rasmi kinathibitisha kwamba kweli kulikuwa na operesheni dhidi ya waasi ambao "wanafanya unyanyasaji na kuwadhulumu watu wanaofanya kazi kwenye migodi". Lakini chanzo hiki kinaongeza kuwa hakna taarifa kuhusu vifo vya raia. Kwa vyovyote vile, operesheni hiyo ya pamoja ilisababisha watu wengi kuhama makazi yao, kimesema chanzo cha usalama.

"Sikujuwa kuhusu shambulio hili," msemaji wa ofisi ya rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati aliliambia shirika la habari la AFP.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca) umefanya mahojiano na manusura ili kujuwa ukweli wa mambo, vimesema vyanzo vya Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.