Pata taarifa kuu
CAR-HAKI

Jamhuri ya Afrika ya Kati: Mahakama Maalum ya Jinai sasa yakamilika

Majaji wa Mahakama Maalum ya Jinai sasa wamekamilika. Mamlaka hii ya mseto inayoundwa na mahakimu wa kitaifa na kimataifa ina jukumu la kushughulikia kesi kuhusiana na uhalifu mbaya zaidi uliofanywa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati tangu mwaka 2003.

Jaji wa Mahakama Maalum ya Jinai (CPS) kutoka Ufaransa Olivier Beauvallet akielekea kuapishwa Jumatano Februari 2 mjini Bangui mbele ya Rais wa Jamhuri Faustin Archange Touadéra.
Jaji wa Mahakama Maalum ya Jinai (CPS) kutoka Ufaransa Olivier Beauvallet akielekea kuapishwa Jumatano Februari 2 mjini Bangui mbele ya Rais wa Jamhuri Faustin Archange Touadéra. © C. Valade/RFI
Matangazo ya kibiashara

Majaji wawili wa mwisho wa kitengo cha rufaa, Olivier Beauvallet kutoka Ufaransa na Volker Nerlich kutoka Ujerumani waliapishwa Jumatano Februari 2 mjini Bangui mbele ya Rais Touadéra.

Hili ni jiwe la mwisho la msingi katika ujenzi wa mradi ulioanzishwa mwaka wa 2015. Miaka sita na nusu baadaye Mahakama Maalum ya Jinai (CPS) imekamilika. Majaji wawili wa mwisho wamekula kiapo mbele ya Mkuu wa Nchi.

Lakini kazi haitakuwa rahisi. Novemba mwaka jana, kiongozi wa zamani wa kivita na ambaye aliteuliwa kuwa waziri Hassan Bouba alikamatwa na Mahakama Maalum ya Jinai, akishtakiwa kwa "uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu". Kwa mshangao mkubwa, aliachiliwa na mamlaka chini ya wiki moja baadaye licha ya kibali cha kukamatwa.

"Sio kwa sababu ya tukio moja la aina hii kwamba tunaweza kuhoji uaminifu wa mahakama, amesema Michel Luanga, jaji mkuu wa Mahakama Maalum ya Jinai (CPS) nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. Nyuma yetu, tunasonga mbele, tuna mengi ya kufanya. »

Lakini kusonga mbele sio kukata tamaa, ameongeza Michel Luanga. “Jalada hili bado halijafungwa, tunaendelea na upelelezi katika jalada hili hivyo nadhani siku zote tuwe na imani na mahakama hii ambayo baada ya miaka michache itajaribu kujibu tatizo la kutoadhibu katika nchi hii. »

 

"2022 ni mwaka muhimu, wa hukumu", ameahidi Jaji mjuu wa Mahakama. Kesi ya kwanza kabisa ya CPS ittangazwa kwa miezi mitatu ya kwanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.