Pata taarifa kuu
CAR-HAKI

CAR: Amnesty yalaani ukosefu wa utekelezaji wa waranti za ICC

Baada ya kuachiliwa kwa Waziri wa Mifugo, Hassan Bouba Ali, ambaye alikuwa amekamatwa kwa amri kutoka kwa Mahakama Maalum ya Uhalifu, mwishoni mwa mwezo Novemba nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Shirika lisilo la kiserikali la Marekani la Amnesty International limepaza sauti na kulaani hatua hiyo.

Toussaint Muntazini Mukimapa (kulia), mwendesha mashtaka wa Mahakama Maalum ya Uhalifu ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, Juni 30, 2017 katika Bunge la kitaifa mjini Bangui.
Toussaint Muntazini Mukimapa (kulia), mwendesha mashtaka wa Mahakama Maalum ya Uhalifu ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, Juni 30, 2017 katika Bunge la kitaifa mjini Bangui. SABER JENDOUBI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Amnesty International inalaani katika taarifa kwamba makumi ya watu wanaoshukiwa kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu bado wako nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Katika taarifa, Amnesty inasema inasikitishwa kwamba kati ya waranti 25 za kukamatwa zilizotolewa na Mahakama Maalum ya Jinai tangu kuundwa kwake mwaka 2015, "ni mmoja tu ndiyo ambayo imeshughulikiwa hadi sasa" baada ya kukamatwa kwa Waziri wa Mifugo wa Afrika ya Kati, Hassan Bouba Ali, Novemba 19.

Lakini haikuchukua muda mrefu. Akishutumiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu, kiongozi huyo wa zamani wa waasi ambaye alikuja kuwa mmoja wa washirika wa rais wa Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadera aliondolewa katika jela ya CPS na maafisa wa kijeshi wa Afrika ya Kati kwa amri ya "mamlaka za Afrika ya Kati na bila uamuzi wowote wa kimahakama ”, shirika hilo la Marekani limelaani.

Kwa sasa, mahakama hii ya mseto kati ya majaji wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na majaji wa kimataifa imeficha majina ya watu wengine 24 ambao wako chini ya waranti wa kukamatwa.

"Baadhi wanaishi mafichoni nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati au nje ya nchi hiyo, lakini wengine hawana wasiwasi," amesikitika Abdoulaye Diara, mtafiti wa shirika la kimataifa la Amnesty International, akibaini kwamba suala la Bouba Ali leo ni "ishara kubwa juu ya matatizo yanayozuia mahakama Maalum ya Jinai, CPS, kufanya kazi kwa kawaida.

Amnesty inatoa wito kwa mamlaka za Jamhuri ya Afrika ya Kati na Umoja wa Mataifa kufanya "uchunguzi wa kweli" unaofuatiwa na "kukata kesi bila kuegemea" dhidi ya wale wote waliohusika na kukiuka sheria za kimataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kwa upande wao, waathiriwa bado wanasubiri "haki, ukweli na fidia", inahitimisha Amnesty.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.