Pata taarifa kuu
CAR-USALAMA

Thelathini na tatu waangamia katika shambulio jipya Jamhuri ya Afrika ya Kati

Takriban watu 33, wakiwemo wanajeshi wawili, waliuawa siku ya Jumatatu (tarehe 29 Novemba) katika mashambulizi yaliyotekelezwa kwa wakati mmoja na watu wenye silaha wanaoshukiwa kuwa waasi wa 3R katika vijiji viwili kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo, katika mkoa wa Ouham-Pendé, nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kikosi cha wanajeshi wa Jmhuri ya Afrika ya Kati, FACA, Januari 10, 2020.
Kikosi cha wanajeshi wa Jmhuri ya Afrika ya Kati, FACA, Januari 10, 2020. © ©AFP - FLORENT VERGNES
Matangazo ya kibiashara

Hii ndiyo idadi kubwa zaidi ya watu waliopoteza maisha tangu rais Faustin Archange Touadéra atangazi kusitishwa kwa mapigano katikati ya mwezi Oktoba.

Waasi wa kundi la 3R wananyooshewa kidole kuhusika na mauaji mengi wanayoendelea kuripotiwa katika eneo hili. Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA inashutumu kundi hili lenye silaha kwa kuwaua raia 12 siku chache zilizopita.

Kuhusu shambulio hili, viongozi katika eneo hilo wamebaini kwamba mashambulizi ni ulipiza kisasi kufuatia kukamatwa kwa gari la mawasiliano la waasi katika eneo hili lililo karibu na mpaka wa Cameroon, na lililoko kilomita 500 kaskazini-magharibi mwa mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui.

Gari hili la mawasiliano lilipatikana msituni Jumapili na lilipelekwa moja kwa moja hadi eneo la Kaïta, kulingana na Naibu Gavana wa mji wa Bocaranga, Isaiah Gbanin. Wakazi wa kijiji hiki kisha walielezea wasiwasi wao kwa mamlaka.

Hofu hii ilithibitishwa siku inayofuata kwa sababu mamia ya waasi waliokuwa na silaha wakati huo huo walishambulia siku ya Jumatatu mji wa Boy-ngou, ambapo kunapatikana kambi kubwa ya jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati, FACA, kwa miezi miwili, na Kaïta, ambako kuna kikosi kidogo cha wanajeshi.

Wakazi wakimbilia Cameroon

Kulingana na shuhuda zilizokusanywa na afisa huyo wa serikali, waasi hao walianzisha mashambulizi yao ya kushtukiza kuanzia saa kumi Alfajiri.Kundi moja liliwashambulia wanajeshi wa FACA huku kundi lingine likiwashambulia raia. Washambuliaji hatimaye walirudi msituni mwendo wa saa  nne asubuhi, na kuacha miili ya raia 29 waliouawa kinyama huko Kaïta, ikiwa ni pamoja na raia wengine 2 na wanajeshi wawili waliouawa huko Boy-ngou, kulingana na mkuu wa mkoa.

Tangu wakati huo, Kaïta, ambayo inajiandaa kuwa mji mkuu wa wilaya ya Lacrenon, ilijikuta wakazi wake zaidi ya 8,000 wakiutoroka mji huo, huku watu 1,000 wakitoroka mji wa Boy-ngou. Wote walipata hifadhi katika nchi jirani ya Cameroon, hasa katika eneo la Yamba. "Kwa sasa, hawataki kurejea katika vijiji vyao wanakotoka kwa kuhofia kuuawa na kundi la waasila 3R kwa ulipizaji kisasi," aMEsema Isaiah Gbanin.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.