Pata taarifa kuu

CAR: Ofisi ya mashtaka yafungua uchunguzi kuhusu kukamatwa kwa wanajeshi 4 wa Ufaransa

Mahakama kuu ya Bangui imeamua kufungua uchunguzi kufuatia kukamatwa kwa wanajeshi wanne wa Ufaransa Jumatatu Februari 21 katika uwanja wa ndege wa Bangui. Tangazo hilo lilitolewa Jumanne Februari 22 na taarifa ilisomwa kwenye redio ya taifa na mwendesha mashtaka wa umma, Laurent Lengande, zaidi ya saa 24 baada ya tukio hilo. Walinda amani wanne bado wanashikiliwa na Umoja wa Mataifa unataka wachiliwe.

Wanajeshi wa Ufaransa waliokamatwa Jumatatu Februari 21, 2022 huko Bangui ni kutoka kikosi cha Minusca.
Wanajeshi wa Ufaransa waliokamatwa Jumatatu Februari 21, 2022 huko Bangui ni kutoka kikosi cha Minusca. AFP/Florent Vergnes
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya usalama vilivyowekwa karibu na uwanja wa ndege kwa ajili ya kuwasili kwa Rais Touadéra, vilishuku gari moja lililosajiliwa nchini Jmahuri ya Afrika ya Kati, ambalo lilikuwa limepewa kwa muga mkuu wa vikosi vya Minusca kwa kusubiri gari lake rasmi. "Gari liliokuwa likifuatiliwa na idaya ya upelelezi kwa miezi miwili", mwendesha mashtaka wa amebaini.

Gari ndogo aina ya Hilux 4x4 nyeusi isiyo na alama

Katika gari hilo kulikuwa na askari kutoka jeshi la Ufaransa, Italia, Bulgaria na Romania kulingana na mwendesha mashtaka. "Timu ya ulinzi wa karibu ya Mkuu wa vikosi vya jeshi la Minusca", Ufaransa na Umoja wa Mataifa wamesema. Ilukuwa timu yenye jukumu la kumsindikiza Jenerali Stéphane Marchenoir alipokuwa akiondoka kuelekea Paris. Mwendesha Mashtaka Lengande anashangaa kuwaona wakitumia gari aina ya 4x4 nyeusi isiyokuwa na alama, yenye vioo vyeusi na ambayo ina usajili wa Jmhuri ya Afrika ya Kati, badala ya magari meupe yenye mhuri wa Umoja wa Mataifa. Mwendesha mashtaka amebaii kwamba katika gari hilo kulikamatwa bastola nne, bunduki tatu za kivita pamoja na bunduki ndogo na mabomu.

Picha za wanajeshi na vifaa vyao zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii Jumatatu jioni, zikiambatana na shutuma za "jaribio" la kumuua rais wa Afrika ya Kati, ambapo Ufaransa na Minusca zinashutumu kampeni ya upotoshaji. Mamlaka nchini Jmhuri ya Afrika ya Kati hadi sasa imekataa kuzungumzia kesi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.