Pata taarifa kuu

Senegal: Operesheni ya kijeshi Casamance yasababisha maelfu ya watu kukmbilia Gambia

Ni takriban wiki moja sasa tangu jeshi la Senegal lianze operesheni ya kijeshi huko Casamance, kusini mwa nchi hiyo. Tangu Jumapili Machi 13, operesheni hii inalenga kwa mujibu wa makao makuu ya jeshi kusambaratisha kambi za kundi la MFDC la kiongozi wa waasi Salif Sadio. N vigumu kupata habari juu ya maendeleo ya operesheni ya kijeshi. Mapigano ya hivi majuzi yamesababisha kuhama kwa watu katika eneo la mpaka.

Mamlaka ya Senegal imeanzisha operesheni dhidi ya waaasi wa Movement for the Democratic Forces of Casamance (MFDC). Hapa, mmoja wa wapiganaji wa kundi hilo, wakati wa kuachiliwa kwa wanajeshi wa Senegal waliotekwa, huko Baipai, Gambia, Februari 14, 2022.
Mamlaka ya Senegal imeanzisha operesheni dhidi ya waaasi wa Movement for the Democratic Forces of Casamance (MFDC). Hapa, mmoja wa wapiganaji wa kundi hilo, wakati wa kuachiliwa kwa wanajeshi wa Senegal waliotekwa, huko Baipai, Gambia, Februari 14, 2022. AFP - MUHAMADOU BITTAYE
Matangazo ya kibiashara

Takriban wakimbizi 6,350 wameorodheswa kwa jumla katika eneo la Foni Kansala kusini mwa Gambia. Hizi ni takwimu za kwanza kutangazwa na idara ya kitaifa ya Kudhibiti Migogoro mjini Banjul tangu kuanza kwa operesheni ya kijeshi.

Miongoni mwao, idadi kubwa ya wakimbi hao - 4,508 - ni wakimbizi wa ndani, ambao ni raia wa Gambia. "Asilimia 61 ya kaya zinaongozwa na wanawake", imeongeza idara hiyo, ambayo inabaini kwamba "watu hawa hawawezi tena kukaa majumbani mwao kwa sababu mapigano yanayoripotiwa karibu na makazi yao na athari za jumla za mapigano yanayoendelea".

Takwimu nyingine: Kaya 543 hazipati msaada wowote. "Katika mpaka wa Senegal na Gambia, ni familia zilezile," anasema mkazi wa eneo hilo, "wanakijiji wengi mara nyingi hupokelewa na wazazi wao" kusini mwa Gambia.

Kwa takriban wiki moja, shuhuda zimeripoti mashambulizi ya anga na ufyatulianaji risasi kaskazini mwa Casamance. Mjini Dakar, makao makuu ya jshi hayatoi maoni yoyote kuhusu maendeleo ya operesheni kwa wakati huu, na haitoi idadi ya vifo au waliojeruhiwa.

Operesheni hii inafuatia mapigano yaliyotokea mwishoni mwa mwezi wa Januari kati ya wapiganaji wanaotaka kujitenga na kikosi cha ECOWAS kutoka Senegal nchini Gambia, kilichopo nchini humo tangu mwaka 2017. Wanajeshi wanne waliuawa, na wengine saba walizuiliwa , hadi walipoachiliwa huru Februari 14.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.