Pata taarifa kuu

Gambia yakabiliwa na wimbi la watu waliokimbia makazi yao kutoka Casamance

Nchini Gambia, idadi ya watu waliokimbia makazi yao na wakimbizi inaendelea kuongezeka baada ya kuanza Jumapili Machi 13 kwa operesheni kubwa ya jeshi la Senegal, kaskazini mwa Casamance.

Mamlaka ya Senegal imeanzisha operesheni dhidi ya wanaharakati wanaotaka kujitengakutoka kundila Movement for the Democratic Forces of Casamance (MFDC). Huu hapa ni mmoja wa wapiganaji wa kundi hilo, wakati wa kuachiliwa kwa wanajeshi wa Senegal waliotekwa, huko Baipai, Gambia, Februari 14, 2022.
Mamlaka ya Senegal imeanzisha operesheni dhidi ya wanaharakati wanaotaka kujitengakutoka kundila Movement for the Democratic Forces of Casamance (MFDC). Huu hapa ni mmoja wa wapiganaji wa kundi hilo, wakati wa kuachiliwa kwa wanajeshi wa Senegal waliotekwa, huko Baipai, Gambia, Februari 14, 2022. AFP - MUHAMADOU BITTAYE
Matangazo ya kibiashara

Tangu mwishoni mwa juma, jamii nyingi zimekuwa zikipokea watu waliokimbia milipuko na milio ya risasi, hasa huko Bujingha, katika wilaya ya Foni, upande wa mpaka wa Gambia.

 

Kilomita chache kutoka mji wa Bwiam, kusini mwa Gambia, kijiji kidogo cha Bujingha kimekuwa kikiwapa hifadhi watu hao tangu Jumamosi Machi 12 karibu watu mia moja waliokimbia makazi kutoka vijiji vinne karibu na mpaka.

Katika kijiji hiki, watu waliolazimika kuyatoroka makazi yao wanalala katika chumba kimoja, kwenye sakafu. Lakini, anavyoeleza Tuti, watu wako tayari kukimbia, tena, iwapo mapigano yataendelea kukaribia kijiji hiki: “Ndiyo maana tunatayarisha chakula chetu mapema sana ili tule kisha tusubiri na kujiandaa. “Tukisikia kelele nyingine, tofauti na wengine, tutafanya shughuli zetu na kwenda kijiji kingine. Hali ambayo haijawahi kutokea

Kwa upande wa chifu wa kijiji, Ismaila Bojang amesema, hali hii haijawahi kushuhudiwa: “Sijawahi kuona hili huko nyuma, chini ya serikali zilizopita. Nchi nzima imechafuka. »

Kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu, ambalo hutoa msaada wa vifaa, limebaini kwamba, zaidi ya watu elfu moja wameondoka kijijini mwao karibu na mpaka. Shirika hilo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wanasaidia mamlaka ya Gambia kufanya tathmini ya hali ilivyo kwa siku mbili. Alhamisi, mkutanobkati ya pande zote utafanyika ili kuweka mkakati wa kuwasaidia watu waliokimbia makazi yao na wakimbizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.