Pata taarifa kuu
SENEGAL-HAKI

Senegal: Adji Sarr avunja ukimya mwaka mmoja baada ya shutuma zake dhidi ya Ousmane Sonko

Nchini Senegal, Adji Sarr amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya kukaa kimya kwa karibu mwaka mmoja. Mnamo Februari 3, 2021, msichana huyo anayefanya kazi ya kumasaji alimshtaki Ousmane Sonko, kiongozi mkuu wa upinzani, kwa kumbaka mara kwa mara.

Adji Sarr.
Adji Sarr. © AS 2022
Matangazo ya kibiashara

Ousmane Sonko ambaye pia ni kiongozi wa chama cha Pastef, amekuwa akikanusha madai hayo akisema kuwa ni njama ya kisiasa. Kesi ya kimahakama ambayo ilisababisha ghasia na vifo 13.

Adji Sarr ambaye amekuwa akizungumza akionyesha tattoo ya hivi majuzi iliyochorwa kwa jina lake la kwanza kwenye kifundo cha mkono. "Kila mtu aliniambia nibadilishe jina langu, ili nisitambulike tena, lakini nilikataa, kwa sababu najivunia kuwa hivi nilivyo", amesema msichana huyo, ambaye alimshutumu mpinzani wa kisiasa Ousmane Sonko mnamo mwaka wa 2021 kwa kumbaka mara kwa mara sehemu alikokuwa akifanyia kazi.

Kesi hii ya mahakama ilizua sintofahamu nchini Senegal, na kusababisha ghasia na vifo kote nchini, wakati kiongozi wa chama cha Pastef alishutumu njama ya kutaka kumuondoa katika ulingo wa kisiasa. Kwa jumla, watu 13 waliuawa kulingana na takwimu rasmi na 590 waliojeruhiwa kulingana nashirika la Msalaba Mwekundu. Mwaka mmoja baadaye, Adji Sarr ameamua kuvunja ukimya "ili ukweli ujulikane", akifanya mahojiano na vyombo kadhaa vya habari.

Mwezi wa Januari 2022 Ousmane Sonko alichaguliwa kuwa meya wa Ziguinchor, moja ya miji mikubwa kusini mwa nchi, na anajiandaa kwa uchaguzi wa wabunge mwezi wa Julai na wakati ni mmoja wa viongozi wakuu wa muungano wa upinzani Yewwi Askan Wi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.