Pata taarifa kuu
CHAD-MAZUNGUMZO

Mazungumzo ya awali ya Chad yashindwa kuanza tena mjini Doha, Qatar

Mazungumzo ya awali ya Chad bado hayajaanza tena mjini Doha nchini Qatar kati ya serikali na makundi ya kisiasa na kijeshi. Mazungumzo hayo yamesitishwa kutokana na sababu nyingi. Washiriki wanaendelea kujadili kuhusu wajumbe watakaowapendekeza.

Washiriki wa mashauriano ya kabla ya mazungumzo wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar katika uzinduzi wa mazungumzo hayo mjini Doha, Machi 13, 2022.
Washiriki wa mashauriano ya kabla ya mazungumzo wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar katika uzinduzi wa mazungumzo hayo mjini Doha, Machi 13, 2022. AFP - KARIM JAAFAR
Matangazo ya kibiashara

Mmoja wa washiriki aliyenukuliwa na shirika la utangazaji la VOA kitengo cha Afrika siku ya Jumamosi amesema kuwa mazungumzo ynaweza kuanza tena Jumapili au Jumatatu, lakini tarehe kamili bado haijajulikana.

Mazungumzo ya awali yalisitishwa muda mfupi baada ya kufunguliwa kwa kikao Jumapili iliyopita nchini Qatar. Katika suala hili: hoja kadhaa za mzozo kwenye ajenda ya mazungumzo ikiwa ni pamoja na suala la idadi ya wawakilishi wa makundi 52 ya kisiasa na kijeshi yaliyopo Doha. Qatar, ambayo ni mpatanishi, ilikuwa imewapa saa 72 kuteua wajumbe kumi ambao wataongoza mazungumzo wakati wa kabla ya mazungumzo.

Makundi ya kijeshi na waaasi yaligawanywa katika makundi mawili: lile la "Roma", kati ya makundi 22 ambayo tayari yalikutana chini ya mwamvuli wa jumuiya ya Sant Egidio kabla ya kwenda Doha. wengine ni "kundi la Doha" linalojumuisha karibu makundi thelathini.

Shughuli zinatazamiwa kuanza tena siku ya Jumatano, lakini wakati huu ni serikali ambayo ilikuwa imeomba muda wa maandalizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.