Pata taarifa kuu

Mazungumzo ya awali ya Chad nchini Qatar: Makundi yenye silaha yashindwa kuchagua wajumbe wao

Ili mazungumzo ya Doha yaanze tena, serikali pamoja na makundi yenye silaha lazima yakubali kuteua wajumbe kumi. Na, kwa upande wa makundi yenye silaha, kwa sasa hakuna makubaliano.

Ufunguzi wa mazungumzo ya awali kati ya serikali na kundi ya kisiasa na wapiganaji nchini Chad, huko Doha, Qatar, Jumapili Machi 13, 2022.
Ufunguzi wa mazungumzo ya awali kati ya serikali na kundi ya kisiasa na wapiganaji nchini Chad, huko Doha, Qatar, Jumapili Machi 13, 2022. © Florence Morice/RFI
Matangazo ya kibiashara

"Mazungumzo ni magumu", amekiri mmoja wa washiriki. "Magumu kabisa na tumeshindwa kufikia makubaliano ya kuwateua wajumbe", mwingine ameongeza. "Tunakimbizana na wakati," mshirika watatu amesema. Mara tu yalipofunguliwa, mazungumzo ya awali kati ya wadau nchini Chad yaliyoandaliwa nchini Qatar yalisitishwa kwa sababu ya watu wengi waliotaka kushiriki katika mazungumzo. Kwa hivyo, tangu Jumapili alasiri, makundi ya kisiasa na wapiganaji yamekuwa vikiendesha vikao vya kazi kujaribu kuwateua pamoja wajumbe kumi ambao lazima wawawakilishe.

Lakini kazi hiyo si rahisi. Hivi sasa, makundi 52 ya kisiasa na wapiganaji yanawakilishwa huko Doha. Wengine wana uzito kuliko wengine kisiasa na kijeshi na sio wote wana ajenda au malengo sawa. Kwa upande mwingine, wote wanataka kuhakikisha kwamba sauti yao inasikika.

"Tunajadili kuhusu tofauti zetu"

Jumatatu jioni, makundi makuu ya waasi yalikuwa hatajitambui: "Kwamba mazungumzo yametakuwa magumu, ni jambo la kawaida kabisa katika mkutano wa aina hii", anasema moja wa washiriki. "Lakini tunajadili kuhusu tofauti zetu," ameongeza.

Qatar inaona kuwa hatua hii ni muhimu, kwani inaona kwamba haiwezi kutekeleza vyema nafasi yake ya mpatanishi na zaidi ya watu mia moja kwenye meza moja. Mashauriano kati ya makundi yaliyojihami yanatazamiwa kuanzishwa tena Jumanne kwa lengo la kuwateua wajumbe kumi kabla ya Jumatano asubuhi ili mazungumzo yaanze tena.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.