Pata taarifa kuu

Urusi kuendelea kuipatia Ulaya gesi licha ya kuripotiwa kwa mzozo

Nchi kubwa zinazouza gesi nje zilikutana Jumanne huko Doha, mji mkuu wa Qatar. Mkutano ambao unakuja katikati ya mzozo wa Ukraine huku Ulaya ikijaribu kubadilisha vifaa vyake.

Marais, mawaziri wakuu au mawaziri wa nchi kumi na moja wanachama wa Jumuiya ya Nchi Zinazouza Gesi (GECF) walikutana mjini Doha, huku mzozo kati ya Moscow na nchi za Magharibi ukichangia kupanda kwa bei.
Marais, mawaziri wakuu au mawaziri wa nchi kumi na moja wanachama wa Jumuiya ya Nchi Zinazouza Gesi (GECF) walikutana mjini Doha, huku mzozo kati ya Moscow na nchi za Magharibi ukichangia kupanda kwa bei. REUTERS - IMAD CREIDI
Matangazo ya kibiashara

Urusi itaendelea kuipatia Ulaya gesi. Hii ni mojawapo ya ahadi kuu zilizotolewa na Waziri wa Nishati wa Urusi wakati wa Kongamano la Nchi Zinazouza Nje Gesi (GECF*) lililofanyika Jumanne Februari 22 huko Doha, nchini Qatar. Nikolai Shulguinov alihakikisha kwamba "makampuni ya Urusi (yalijitolea) kikamilifu kwa mikataba iliyopo". Bila kutaja mgogoro kati ya Urusi na nchi za Magharibi.

"Msaada"

Kwa upande wake, Qatar ilikumbusha "msaada" wake kwa Ulaya ikiwa kutatokea matatizo ya usambazaji. Qatar, ambayo ni muuzaji mkubwa zaidi wa gesi asilia iliyoyeyuka duniani, inaweza kutumika kama chanzo mbadala cha usambazaji. Lakini usafirishaji wake hadi sasa unakusudiwa kwa nchi za Asia.

"Ugavi wa kuaminika"

"Tunashukuru juhudi za wanachama wote wa (GECF) ambao wamefanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha usambazaji wa kuaminika wa gesi asilia kwenye soko la kimataifa na kuhifadhi utulivu wa masoko haya," Kiongozi wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani alisema mbele ya washiriki. Mgogoro huo unachangia kuongezeka kwa bei katika sekta hiyo.

* GECF: Qatar, Urusi, Iran, Bolivia, Misri, Equatorial Guinea, Libya, Nigeria, Trinidad na Tobago, Venezuela na nchi saba zinazohusiana kwa pamoja zinawakilisha zaidi ya 70% ya hifadhi ya dunia na 51% ya mauzo ya gesi ya asilia iliyoyeyuka duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.