Pata taarifa kuu
UKRAINE-USALAMA

DRC: Wanafunzi kumi na wawili wa DRC waondoka kaskazini-mashariki mwa Ukraine

Jumanne, Machi 8, kutokana na maeneo salama ya kiutu, wanafunzi kumi na wawili wa DRC waLIweza kuondoka Chuo Kikuu cha Sumy, kaskazini-mashariki mwa Ukraine ambayo inayokabiliwa na mashambulizi ya Urusi.

Wanafunzi wa Kiafrika wakimbizi kutoka Ukraine huko Przemysl mashariki mwa Poland. Februari 28, 2022.
Wanafunzi wa Kiafrika wakimbizi kutoka Ukraine huko Przemysl mashariki mwa Poland. Februari 28, 2022. AFP - WOJTEK RADWANSKI
Matangazo ya kibiashara

Kwa siku kadhaa, vijana wa Kiafrika wamenaswa katika mzozo huu kati ya Ukraine na Urusi. Raia hawa kumi na wawili kutoka DRC sasa wako salama magharibi mwa nchi.

Wanafunzi hao sasa wako salama Ternopil, kilomita 200 kutoka mpaka wa Poland. Wakongo hawa kumi na wawili, kwa sehemu kubwa, ni wanafunzi wanaosomea elimu ya matibabu. Wameweza kuondoka Sumy kwa teksi.

Zaidi ya euro 900, ni kifedha ambazozlilipwa kama nauli kwa wanafunzi hao, kiwango cha fedha ambacho kimezidishwa karibu mara 20 kwa sababu ya mgogoro. Fedha hizo zimelipwa na serikali ya DRC.

Vijana hao walikuwa waliwasili kwanza Poltava, kusini mwa Ukraine, ambapo walichukua treni hadi mji wa Ternopil.

Tangu kuwasili kwao Jumanne, wamekaribishwa na raia mmoja wa DRC anayeitwa Serge Nyangi Mamputu, mjasiriamali mwenye moyo mkunjufu aliyefuata kuhamishwa kwao tangu mwanzo hadi mwisho.

Kwa upande wengine serikali ya DRC imesema iko tayari kuendelea kuwaunga mkono.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.