Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine vyazua hisia za tahadhari barani Afrika

Urusi ilianza uvamizi dhidi ya Ukraine Alhamisi hii, Februari 24, uvamizi uliyolaaniwa kwa kauli moja na nchi za Magharibi. Nchi nyingi za Afrika zinasita kutoa msimo ulio thabiti.

Rais wa Senegal na Mwenyekiti wa AU Macky Sall ameelezea wasiwasi wake kuhusiana na hali nchini Ukraine. Hapa, ni wakati alipowasili katika siku ya kwanza ya mkutano wa kilele wa AU na EU, Februari 17, 2022.
Rais wa Senegal na Mwenyekiti wa AU Macky Sall ameelezea wasiwasi wake kuhusiana na hali nchini Ukraine. Hapa, ni wakati alipowasili katika siku ya kwanza ya mkutano wa kilele wa AU na EU, Februari 17, 2022. AFP - JOHN THYS
Matangazo ya kibiashara

Jioni ya shambulio la Urusi dhidi ya Ukraine, nchi nyingi barani Afrika zimekuwa bado zikijizuia kuonyesha msimamo wao. Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Macky Sall na yule wa Tume ya umoja huo, Moussa Faki Mahamat, wote walionyesha "wasiwasi wao kuhusiana na hali mbaya na hatari nchini Ukraine". Wanatoa wito kwa Urusi na wahusika wengine wote kuheshimu sheria ya kimataifa, uadilifu wa eneo na uhuru wa Ukraine. Wanazitaka pande zote mbili kuanzisha mara moja usitishaji vita na kufungua mazungumzo ya kisiasa bila kuchelewa.

Algeria, mshirika wa kihistoria wa Urusi, imetoa wito kwa raia wake walio nchini Urusi kuwa waangalifu sana bila hata hivyo kuonyesha msimamo wake.

Hata hivyo Afrika Kusini pekee, ndiyo nchi pekee barani Afrika imeonyesha msimamo wake kwa kuelezea wasiwasi wake juu ya uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine. Moscow inachukuliwa kuwa mshirika wa kimkakati wa Afrika Kusini, mwanachama kama Pretoria wa jumuiya ya kiuchumi ya BRICS. Pia ni mshirika wa muda mrefu wa ANC, chama tawala, wakati USSR ya zamani iliunga mkono harakati za ukombozi kusini mwa Afrika.

Serikali ya Afrika Kusini sasa inadai kuondolewa mara moja kwa wanajeshi wa Urusi nchini Ukraine.

Lakini msimamo huu unachukuliwa na baadhi kuwa umechelewa sana, anaripoti mwandishi wetu wa Johannesburg, Romain Chanson. Mkuu wa masuala ya kimataifa wa chama cha upinzani cha Democratic Alliance, Darren Bergman, anasikitika kwamba serikali imeonyesha kujizuia sana hadi sasa. "Wanaonekana kujizuia na kukata kutamka kauli yoyote itayoikwaza Urusi. Ni wazi kwamba wanaheshimu mshirika wao wa BRICS na kubaki na nidhamu. Afadhali tunapaswa kutumia uhusiano wetu katika Brics kulaani Urusi kwa maneno makali, "amesema.

Afrika Kusini inasema inaheshimu uhuru na uadilifu wa eneo la nchi. Lakini pia inasema kwamba suluhu la kidiplomasia lazima lipatikane kwa wasiwasi uliotolewa na Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.